125-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 125: وَاتَّخِذُوا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah 125: na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia...

 

 

وَإِذْ جَعَلْنَا الْبَيْتَ مَثَابَةً لِّلنَّاسِ وَأَمْنًا وَاتَّخِذُوا مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى ۖ وَعَهِدْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ ﴿١٢٥﴾ 

125. Na Tulipoifanya Nyumba (Al-Ka’bah) kuwa ni mahali pa kurejewa na watu na pa amani, na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia. Na Tulichukua ahadi kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl kwamba: “Itakaseni Nyumba Yangu kwa wanaotufu na wanaokaa i’tikaaf, na wanaorukuu na kusujudu.”

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii: “Na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia”, iliteremka pale ‘Umar (رضي الله عنه) alipomwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Lau tungelifanya sehemu aliyosimama Ibraahiym kuwa ni sehemu ya kuswalia.” Kisha baada ya hapo ikateremka Aayah hii. [Al-Bukhaariy kwa ufupi kutoka kwa ‘Umar] Na sehemu aliyosimama Ibraahiym ndiyo iitwayo Hijri.

 

 

Hadiyth kamili:

 

 عَنْ أَنَسٍ، قَالَ قَالَ عُمَرُ: وَافَقْتُ رَبِّي فِي ثَلاَثٍ، فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ لَوِ اتَّخَذْنَا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى فَنَزَلَتْ: ((‏وَاتَّخِذُوا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى))‏ وَآيَةُ الْحِجَابِ،  قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، لَوْ أَمَرْتَ نِسَاءَكَ أَنْ يَحْتَجِبْنَ، فَإِنَّهُ يُكَلِّمُهُنَّ الْبَرُّ وَالْفَاجِرُ‏.‏ فَنَزَلَتْ آيَةُ الْحِجَابِ، وَاجْتَمَعَ نِسَاءُ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي الْغَيْرَةِ عَلَيْهِ فَقُلْتُ لَهُنَّ عَسَى رَبُّهُ إِنْ طَلَّقَكُنَّ أَنْ يُبَدِّلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِنْكُنَّ‏.‏ فَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ‏

Kutoka kwa ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Rabb Wangu Ameniwafikia mambo matatu: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Lau tungefanya sehemu aliyosimamia Ibraahiym kuwa sehemu ya kuswali. Ikateremka: “na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia.” (2: 125) Na Aayah ya hijaab nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Ungewaamrisha wake zako kujiwekea hijaab (kizuizi) kutokana na wanaume kwa sababu watu wema na waovu wanaongea nao. Basi ikateremka Aayah ya hijaab kwa wanawake. Na wakeze Nabiy walijiunga dhidi ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na wivu wao baina yao. Nikawaambia: Huenda akutalikini kisha Rabb wake Ambadilishie wake walio bora zaidi kuliko nyinyi” ikateremka Aayah (At-Tahriym  5)  [Al-Bukhaariy]

 

Share