Mkate Wa Boflo Wa Maziwa (Loaf)

Mkate Wa Boflo  Wa Maziwa (Loaf)

Vipimo

Kipimo cha mikate miwili

Unga mweupe - 6 vikombe (29 ounces takriban)

Hamira - 2 vijiko vya chai

Siagi (butter) - 2 Vijiko vya kulia

Maji ya dafudafu (warm) - 1 kikombe

Maziwa dafudafu - 1 kikombe

Sukari - 2 Vijiko vya kulia

Chumvi - 1 kijiko cha chai

 Namna Ya Kutayarisha Na Kupika    

  1. Weka katika bakuli la mashine (electrical bowl) hamira, maziwa, sukari chumvi na siagi iliyoyaushwa. Changanya vizuri kwa mwiko.
  2. Tia unga pole pole huku umeasha mashine ikande,  ukiongezea unga mpaka umalizike.
  3. Pakaza siagi bakuli jengine kubwa kisha mimina mchanganyiko. Funika kwa kitambaa kilichokuwa kimeloa maji (damp cloth) au karatasi ya plastiki (plastic wrap). Uache unga uumuke mpaka uwe  saizi ya mara mbili yake.
  4. Utoe hewa unga na umimine juu ya baraza (flat surface). Gawa mchanganyiko sehemu mbili umimine katika treya ya loaf (loaf pan) size ya treya 9 x 5 inchies takriban.  Acha uumuke tena kiasi nusu saa.
  5. Washa oveni mapema kiasi 200 Degrees uchome (bake) kaisi nusu saa mpaka ugeuke rangi ya hudhurungi (golden brown).
  6. Epua upoe ukiwa tayari.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

Share