Imaam Ibn Baaz: Haifai Kuswali Kwenye Miswala Au Mazulia Yenye Picha Ya Ka’bah Na Masjid An-Nabawiy

Haifai Kuswali Kwenye Miswala Au Mazulia Yenye Picha

Ya Ka’bah Na Masjid An- Nabawiy

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Tunaona baadhi ya mazulia ya kuswalia yana picha za Ka’bah au picha ya Masjid Nabawiy juu yake. Je, nini hukumu ya kuswalia?

 

 

JIBU:

 

Mazulia (Miswala) haya yasiswaliwe kwa sababu kusimamia Ka’bah kwa miguu yako ni aina ya kuidunisha (kuidhalilisha).  Hairuhusiwi kuweka picha za Ka’bah juu ya Mazulia (au Miswala) na haipasi kuinunua.

Kwa sababu ikiwa mbele yake (anaposwalia) inamshughulisha mtu, na ikiwa iko chini ya miguu (anaikanyagia), basi hivyo kuidharau.

Kwa hiyo ili Muumini asalimike, hapasi kutumia mazulia (na miswala) hiyo.

 

[Fataawa Ibn Baaz​, http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=37061]

 

 

 

 

 

Share