Choka: Sosi Ya Bilingani Vitunguu Na Nyanya Ya Kuchomwa - Grilled (Trinidad)

Choka: Sosi Ya Bilingani Vitunguu Na Nyanya Ya Kuchomwa - grilled (Trinidad)

Vipimo

 

 

Bilingani - 2

Kitunguu - 2

Nyanya - 5

Kotmiri - 1 msongo (bunch)

Mafuta ya zaituni (olive oil) - ¼  kikombe

Thomu (garlic/somu) katakakata au kuna - 7 chembe

Pilipili mbichi kijani - 2

Chumvi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Kata bilingani vipande vidogo kiasi.  Katakata nyanya/tungule changanya na bilingani kisha weka katika bakuli la kupikia ndani ya oveni.
  2. Nyunyizia mafuta ya zaituni kiasi vijiko vitatu vya kulia. Kisha weka kwenye oveni uchome (bake) kwa muda wa dakika 15 takriban moto wa kiasi 250-300 degrees. 
  3. Kisha zima moto na washa moto wa juu kisha aaha ichomeke kiasi tena dakika 15-20 huku unachanganya ili nyanya na bilingani zichomeke moto wa juu  (grill).
  4. Epua, kisha kataka vitunguu slaisi, katakata pilipili mbichi au saga. Kuna thomu au saga, katakata kotimiri. Changanya katika bakuli hilo. Tia chumvi.
  5. Pasha moto mafuta yaliyobakia yashike moto kisha mwagia juu yake, changanya ikiwa tayari kama kitoleo. 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Kidokezo: 

Aghlabu huliwa na viazi vitamu vya kuchemsha au viazi vya kawaida, au mikate.

 

 

 

 

 

 

Share