198-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 198: لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَنْ تَبْتَغُوا فَضْلاً مِنْ رَبِّكُمْ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Al-Baqarah Aayah 198: Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Rabb wen
لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَبْتَغُوا فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ ۚ فَإِذَا أَفَضْتُم مِّنْ عَرَفَاتٍ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ عِندَ الْمَشْعَرِ الْحَرَامِ ۖ وَاذْكُرُوهُ كَمَا هَدَاكُمْ وَإِن كُنتُم مِّن قَبْلِهِ لَمِنَ الضَّالِّينَ ﴿١٩٨﴾
198. Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Rabb wenu. Basi mtakapomiminika kutoka ‘Arafaat mdhukuruni Allaah kwenye Mash’aril- Haraam (Muzdalifah) na mdhukuruni Yeye kama Alivyokuongozeni kwani hakika mlikuwa kabla ya hapo ni miongoni mwa waliopotea.
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii: “Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Rabb wenu”, imeteremka kuhusu Maswahaba kuwa waliona uzito kufanya biashara kwenye masoko yaliyokuwa yakitumika zama za Jaahiliyyah. Ndipo ikateremka Aayah hii. [Al-Bukhaariy kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)] Hadiyth kamili:
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضى الله عنهما قَالَ : كَانَتْ عُكَاظٌ وَمَجَنَّةُ وَذُو الْمَجَازِ أَسْوَاقًا فِي الْجَاهِلِيَّةِ فَتَأَثَّمُوا أَنْ يَتَّجِرُوا فِي الْمَوَاسِمِ فَنَزَلَتْ: ((لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَنْ تَبْتَغُوا فَضْلاً مِنْ رَبِّكُمْ)) فِي مَوَاسِمِ الْحَجِّ.
Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ambaye amesema: ‘Ukaadhw, na Majannah na Dhul-Majaaz yalikuwa masoko wakati wa Jaahiliyyah (kabla ya Uislamu). Basi (Waislamu) waliodhania ni dhambi kufanya biashara katika msimu (wa Hajj), ndipo ikateremka: “Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Rabb wenu…”katika misimu ya Hajj [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr, Kitaab Al-Buyuw’, pia Sunan Abiy Daawuwd Kitaabu Al-Manaasik]