199-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 199: ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah 199: Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu;

 

 

  ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٩٩﴾

199. Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu; na ombeni maghfirah kwa Allaah. Hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii: “Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu;” imeteremka kuhusu Maquraysh kwa vile wao walikuwa wakimiminika kutokea Muzdalifah na hali ya kuwa watu wengineo wanamiminika kutokea ‘Arafah. Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaamrisha nao Maquraysh wamiminike kutokea ‘Arafah kama wafanyavyo wengineo. [Al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها)]

 

Hadiyth zimethibiti katika riwaayah kadhaa. Ama ifuAtayo ni kama ilivyokusanywa na Imaam Al-Bukhaariy katika Kitaab Al-Hajj iliyopokelewa kutoka kwa ‘Urwah (رضي الله عنه):

 

كَانَ النَّاسُ يَطُوفُونَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ عُرَاةً إِلاَّ الْحُمْسَ، وَالْحُمْسُ قُرَيْشٌ وَمَا وَلَدَتْ، وَكَانَتِ الْحُمْسُ يَحْتَسِبُونَ عَلَى النَّاسِ يُعْطِي الرَّجُلُ الرَّجُلَ الثِّيَابَ يَطُوفُ فِيهَا، وَتُعْطِي الْمَرْأَةُ الْمَرْأَةَ الثِّيَابَ تَطُوفُ فِيهَا، فَمَنْ لَمْ يُعْطِهِ الْحُمْسُ طَافَ بِالْبَيْتِ عُرْيَانًا، وَكَانَ يُفِيضُ جَمَاعَةُ النَّاسِ مِنْ عَرَفَاتٍ، وَيُفِيضُ الْحُمْسُ مِنْ جَمْعٍ‏.‏ قَالَ وَأَخْبَرَنِي أَبِي عَنْ عَائِشَةَ رضى الله عنها أَنَّ هَذِهِ الآيَةَ نَزَلَتْ فِي الْحُمْسِ: ((‏ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ‏)) قَالَ كَانُوا يُفِيضُونَ مِنْ جَمْعٍ فَدُفِعُوا إِلَى عَرَفَاتٍ‏.‏

“Wakati wa kipindi cha Ujaahiliyyah, watu walikuwa wakitufu Al-Ka’bah wakiwa uchi isipokuwa Al-Hums. Na Al-Hums walikuwa ni (kabila la) Quraysh pamoja  na kizazi chao. Na Al-Hums walikuwa wakiwapa nguo watu wanaofanya twawaaf ili wazivae na wanawake (wa Al-Hums) walikuwa wakiwapa nguo wanawake waliokuwa wakifanya twawaaf wazivae. Wale ambao Al-Hums hawakuwapa nguo walifanya twawaaf wakiwa uchi. Wengi wa watu walikuwa wakimiminika kutoka ‘Arafah moja kwa moja lakini (Al-Hums) walikuwa wakimiminika kutoka baada ya kukaa Muzdalifah.” ‘Urwah akaendelea kusema: “Baba yangu amehadithia kwamba ‘Aaishah amesema: “Aayah ifuatayo imeteremshwa kuhusu Al-Hums. Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu” (2: 99) ‘Urwah akaendelea kusema: “Wao (Al-Hums) walikuwa wakibakia Muzdalifah na wakiondokea kutoka humo (kwenda Minaa), basi ndio wakageuzwa kuondokea ‘Arafah (kwa amri ya Allaah.”

 

Share