207-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 207: وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْرِي نَفْسَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Al-Baqarah Aayah 207: Na miongoni mwa watu yupo anayeiuza nafsi yake kutafuta
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْرِي نَفْسَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴿٢٠٧﴾
207. Na miongoni mwa watu yupo anayeiuza nafsi yake kutafuta radhi za Allaah. Na Allaah ni Mwenye huruma mno kwa waja
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii: “Na miongoni mwa watu yuko anayeiuza nafsi yake kutafuta Radhi za Allaah”, imeteremka kuhusu Suhayb (رضي الله عنه) pale alipotoka Makkah akiwa ni mwenye kuhamia Madiynah. Watu wa Makkah wakamfuata ili wamrejeshe. Alikuwa amewaacha vijakazi wawili Makkah, basi ili aachiwe kuhajiri kutoka Makkah kwenda Madiynah, aliwapatia hao waliomfuata vijakazi wawili hao. Hapo wakamuachia. [Imaam Al-Haakim kutoka kwa Anas (رضي الله عنه)]