219-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 219: يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 219:  Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema:

 

 

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١٩﴾

219. Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: “Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake.” Na wanakuuliza nini watoe. Sema: “Yaliyokuzidieni.” Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na  shariy’ah) ili mpate kutafakari.

 

Sababun-Nuzuwl

 

Aayah hii imeteremshwa pale 'Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) ambaye alikuwa mmoja wa Swahaba wenye kulewa, siku moja alisema: Ee Rasuli wa Allaah, tupe hukmu kuhusu Al-khamr (pombe). Hapo ikateremka Aayah:

 

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ

Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake. [Al-Baqarah (2:219)]

 

Kisha ikafuatia Aayah (4:43) ya kutokukaribia Swalaah baada ya kulewa.

 

Kisha ikaharamishwa kabisa katika Suwratul-Maaidah (5:90). Rejea huko kupata maelezo bayana.

 

Hadiyth kama ilivyothibiti katika [Sunan Abiy Daawuwd Kitaab Al-Ashribah Baab Tahriym Al-Khamr]

 

عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ، قَالَ لَمَّا نَزَلَ تَحْرِيمُ الْخَمْرِ قَالَ عُمَرُ: اللَّهُمَّ بَيِّنْ لَنَا فِي الْخَمْرِ بَيَانًا شِفَاءً ، فَنَزَلَتِ الآيَةُ الَّتِي فِي الْبَقَرَةِ: ((‏يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ)) الآيَةَ قَالَ: فَدُعِيَ عُمَرُ فَقُرِئَتْ عَلَيْهِ، قَالَ: اللَّهُمَّ بَيِّنْ لَنَا فِي الْخَمْرِ بَيَانًا شِفَاءً، فَنَزَلَتِ الآيَةُ الَّتِي فِي النِّسَاءِ: ((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تَقْرَبُوا الصَّلاَةَ وَأَنْتُمْ سُكَارَى))‏ فَكَانَ مُنَادِي رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا أُقِيمَتِ الصَّلاَةُ يُنَادِي: أَلاَ لاَ يَقْرَبَنَّ الصَّلاَةَ سَكْرَانُ، فَدُعِيَ عُمَرُ فَقُرِئَتْ عَلَيْهِ  فَقَالَ: اللَّهُمَّ بَيِّنْ لَنَا فِي الْخَمْرِ بَيَانًا شِفَاءً فَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ: ((‏فَهَلْ أَنْتُمْ مُنْتَهُونَ))‏ قَالَ عُمَرُ: انْتَهَيْنَا.‏

Imepokelewa kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) kwamba ilipoharamishwa pombe alisema ‘Umar: Ee Allaah tubainishie kuhusu pombe bainisho la kuridhisha.” Hapo ikateremshwa Aayah katika Suwratul-Baqarah:

 

 ‏يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ

Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: “Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa.    

 

[Al-Baqarah 2: 219] Akaitwa ‘Umar akasomewa. Kisha akasema: “Ee Allaah tubainishie kuhusu pombe bainisho la kuridhisha.” Kisha ikateremshwa Aayah katika Suwratun-Nisaa:

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تَقْرَبُوا الصَّلاَةَ وَأَنْتُمْ سُكَارَى

“Enyi waloamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa...” [An-Nisaa 4: 43]

 

Kisha muitaji wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akitangaza  pale inapokimiwa Swalaah: “Tahadharini! Aliyelewa asikaribie Swalaah!” ‘Umar akaitwa tena na akasomewa akasema: “Ee Allaah tubainishie kuhusu pombe bainisho la kuridhisha.” Ikateremka Aayah:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾

Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli, ni najisi na chukizo kutokana na kazi ya shaytwaan. Basi jiepusheni navyo mpate kufaulu. [Al-Maaidah (5:90)]

 

إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾

Hakika shaytwaan anataka kukutilieni baina yenu uadui na bughudha katika pombe na kamari na akuzuieni kumdhukuru Allaah na Swalaah; basi je mtakoma? [Al-Maaidah (5:90-91)]

‘Umar akasema: “Tumekoma.” [Imaam Al-Albaaniy ameisahihisha katika Swahiyh Abiy Daawuwd (3670)]

 

 

 

Share