220-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 220: وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَىٰ ۖ قُلْ إِصْلَاحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Al-Baqarah Aayah 220: Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: “Kuwatengeneza ni kheri.
فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۗ وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَىٰ ۖ قُلْ إِصْلَاحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ ۖ وَإِن تُخَالِطُوهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ الْمُفْسِدَ مِنَ الْمُصْلِحِ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَأَعْنَتَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٠﴾
220. Katika dunia na Aakhirah. Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: “Kuwatengeneza ni kheri. Na mkichanganya mambo yenu na yao basi hao ni ndugu zenu. Na Allaah Anamjua fisadi na mtengenezaji. Na lau Angetaka Allaah Angelikutieni katika shida.” Hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.
Sababun-Nuzuwl:
Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba: Ilipoteremka Aayah: “Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia ya ihsaan”, na pia: “Hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhulma… (4:10), watu wakajiepusha na mali na chakula cha yatima. Ikawa ni ngumu kwao, wakalalamika kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha: “Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: “Kuwatengenezea ni khayr…” (2:220) [Swahiyh An-Nasaaiy (3671), Fathul-Baariy (5/463)]
Hadiyth kama ilivyothibiti:
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ لَمَّا نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ ((وَلاَ تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلاَّ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ)) وَ((إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَى ظُلْمًا)) قَالَ: اجْتَنَبَ النَّاسُ مَالَ الْيَتِيمِ وَطَعَامَهُ فَشَقَّ ذَلِكَ عَلَى الْمُسْلِمِينَ فَشَكَوْا ذَلِكَ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَأَنْزَلَ اللَّهُ: ((وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَى قُلْ إِصْلاَحٌ لَهُمْ خَيْرٌ)) إِلَى قَوْلِهِ ((لأَعْنَتَكُمْ)).
Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba pale Aayah hizi zilipoteremshwa: “Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia ya ihsaan…” [Al-Anaam 152] na, “Hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhulma…” [An-Nisaa: 10], akasema: Watu walijiepusha na mali ya yatima pamoja na chakula chake, ikawa ni mashaka kwa Waislamu wakashitaki kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hapo ikataremka: “Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: “Kuwatengeneza ni kheri…” mpaka kauli Yake: “Angelikutieni katika shida.” [Sunan An-Nasaaiy katika Kitaab Al-Wiswaayaa, Baab maa lil-waswiyyi min maal al-yatiym idhaa qaama ‘alayhi].