222-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 222: وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 222:Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema…  

 

 وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ ﴿٢٢٢﴾ 

222. Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni dhara; basi waepukeni wanawake katika hedhi. Wala msiwakaribie (kujimai nao) mpaka watwaharike. Watakapotwaharika basi waendeeni kupitia pale Alipokuamrisheni Allaah.”  Hakika Allaah Anapenda wenye kutubia na Anapenda wenye kujitwaharisha.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii: Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni dhara; basi waepukeni wanawake katika hedhi,” imeteremka kuwazungumzia Mayahudi ambao walikuwa mwanamke akipatwa na hedhi, hawali nae chakula wala hawajumuiki nae katika majumba. Maswahaba wakamuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu jambo hilo, na hapo ikateremka Aayah hii. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Fanyeni kila kitu isipokuwa jimai.”  [Muslim Hadiyth ya Anas bin Maalik (رضي الله عنه)]

 

 

Hadiyth kama ilivyothibiti:

 

عَنْ أَنَسٍ، أَنَّ الْيَهُودَ، كَانُوا إِذَا حَاضَتِ الْمَرْأَةُ فِيهِمْ لَمْ يُؤَاكِلُوهَا وَلَمْ يُجَامِعُوهُنَّ فِي الْبُيُوتِ فَسَأَلَ أَصْحَابُ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى: ((وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ‏))  إِلَى آخِرِ الآيَةِ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((اصْنَعُوا كُلَّ شَىْءٍ إِلاَّ النِّكَاحَ)) ‏ فَبَلَغَ ذَلِكَ الْيَهُودَ فَقَالُوا: مَا يُرِيدُ هَذَا الرَّجُلُ أَنْ يَدَعَ مِنْ أَمْرِنَا شَيْئًا إِلاَّ خَالَفَنَا فِيهِ. فَجَاءَ أُسَيْدُ بْنُ حُضَيْرٍ وَعَبَّادُ بْنُ بِشْرٍ فَقَالاَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ الْيَهُودَ تَقُولُ كَذَا وَكَذَا فَلاَ نُجَامِعُهُنَّ، فَتَغَيَّرَ وَجْهُ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم حَتَّى ظَنَنَّا أَنْ قَدْ وَجَدَ عَلَيْهِمَا، فَخَرَجَا فَاسْتَقْبَلَهُمَا هَدِيَّةٌ مِنْ لَبَنٍ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَأَرْسَلَ فِي آثَارِهِمَا فَسَقَاهُمَا فَعَرَفَا أَنْ لَمْ يَجِدْ عَلَيْهِمَا ‏.‏

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kwamba Mayahudi walikuwa pale mwanamke anapokuwa katika hedhi hawakuwa wakila naye wala hawajumuiki naye nyumbani mwao. Basi Maswahaba wakamuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Allaah (تعالى) Akateremsha: Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni dhara; basi waepukeni wanawake katika hedhi.” Mpaka mwisho wa Aayah. Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Fanyeni kila kitu (nao) isipokuwa kujamiiana)). Yakawafikia Mayahudi hayo wakasema: “Mtu huyu hataki kuacha lolote ila tu akhitilafiane nasi kwalo.” Akaja Usayd bin Hudhwayr na ‘Abbaadu bin Bishr wakasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Hakika Mayahudi wamesema kadhaa wa kadhaa.  Hivyo basi tusijamiiane nao.” Hapo uso wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ukabadilika mpaka tukadhania kwamba amewakasirikia. Walipotoka nje walipokea hadiya ya maziwa aliyoletewa Nabiy. Akawaita akawagaia kinywaji hicho, hapo wakatambua kuwa kumbe hakukasirika nao. [Muslim katika Kitaab Al-Haydhw]

 

 

Share