46-Kitaab At-Tawhiyd: Kujiita Qadhi Wa Maqadhi Na Mfano Wake

Mlango Wa 46

بَابٌ التَّسَمِّي بِقَاضِي الْقُضَاةِ وَنَحْوِهِ

Kujiita Qadhi Wa Maqadhi Na Mfano Wake


 

 

 

فِي الصَّحِيحِ: عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنِ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((إِنَّ أَخْنَعَ اِسْمٍ عِنْدَ اللَّهِ رَجُلٌ تَسَمَّى مَلَكَ الأَمْلاكِ، لاَ مَالِكَ إِلاَّ اللَّهَ))

Katika Swahiyh Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah(رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Jina ovu na  la kuchukiza mno kwa Allaah ni mtu kujiita MalakAl-Amlaak [mfalme wa milki zote]. Hakuna Maalik isipokuwa Allaah))

 

قَالَ سُفْيَانُ مِثْلُ شَاهَانْ شَاهْ .

Sufyaan amesema: mfano: “Shaahaan Shaah” (mfalme wa wafalme kwa Wafursi).

 

وَفِي رِوَايَةٍ: ((أَغْيَظُ رَجُلٍ عَلَى اللَّهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَأَخْبَثُهُ ))

Na katika riwaayah nyingine:

((Mtu mwenye kuchukiwa mno na muovu kabisa mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah [ni mtu anayejiita: mfalme wa wafalme])) [Al-Bukhaariy]

Na maana ya  أخنع  ni   أوضع:  duni, aliyedhalilika kabisa.

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Kukatazwa kutumia cheo cha ‘mfalme wa wafalme’ kwa yeyote.

 

2-Kukatazwa mfano wake kama mfano uliotolewa na Sufyaan (رضي الله عنه).

 

3-Ufahamu na kuelewa uzito wa kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) licha ya kuwa mtu anaweza asidhamirie maana mbaya moyoni mwake.

 

4-Utambuzi na ufahamu kwamba kutukuzwa kiuabudiwa ni kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee Mtukufu kuliko wote, Asiyefikiwa hata chembe ‘Uluwa Yake, Ametakasika na kila kitu (tofauti na ‘mfalme’ wa kidunia).

 

 

 

 

 

Share