Sitta Shawwaal: Kutia Niyyah Swawm Za Sitta Shawwaal Na Swawm Za Ayyaamul-Biydhw Inajuzu?
Kutia Niyyah Swawm Za Sitta Shawwaal Na Swawm Za Ayyaamul-Biydhw Inajuzu?
SWALI:
Assalam alaykum, swali ni je waweza kulipa deni la ramadhan ndani ya sunna ya yaumul baydhaa (masiku meupe)?
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Ndugu katika iymaan tunashukuru kujua una himma ya kutekeleza ‘ibaadah tukufu kama hizo.
Inajuzu kutia niyyah mbili kwa ajili ya Sittatu Ash-Shawwaal na Swiyaam za Ayyaamul Biydhw kwa kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
“Hakika kusihi kwa ‘amali huzingatiwa na niyyah. Na hakika kila mtu atalipwa kwa kile alichokinuia.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na hivyo pia inafaa kutia niyyah kuzifunga Sittatu Ash-Shawwaal pamoja na Swiyaam za Jumatatu na Alkhamiys.
Jambo ambalo halijuzu pekee kuhusu Swiyaam za Sittatu Ash-Shawwaal ni kuzitilia niyyah pamoja na deni la Ramadhwaan kwa sababu sharti ya kuzifunga Sittatu Ash-Shawwaal ni kuwa lazima mtu awe amekamilisha Swiyaam za Ramadhwaan zote siku 29 au siku 30 kwani faida na hikmah yake inapatikana katika kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba pindi ukimaliza Ramadhwaan kisha ukafuatilia na siku Sita za Shawwaal ndipo utakapopata thawabu za Swiyaam ya mwaka.
Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo kwa faida zaidi:
02-Kulipa Ramadhwaan Au Sita Shawwaal? Inafaa Kulipa Jumatatu Na Alkhamiys
04-Swawm Ya Sitta Shawwaal Jumatatu Na Alkhamiys Kupata Thawabu Niyyah Mbili
Na Allaah Anajua zaidi