Shaykh Fawzaan: Kupitwa Swalaah Ya Alfajiri

 

Kupitwa Swalaah Ya Alfajiri

 

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Muulizaji anasema kuwa hawezi kuamka kuswali Alfajiri, bali huswalia saa moja asubuhi, je atapata dhambi?

 

 

JIBU:

 

Na'am, (atapata dhambi), inamuwajibikia aswali pamoja na Jamaa’ah Swalaah ya Alfajiri kisha ndio alale wala haijuzu kwake kuacha Swalaah ya Jamaa’ah wala haijuzu kumpita wakati wa Swalaah ya Alfajiri, wala kuifanyia upuuzi kwani Allaah Haikubali Swalaah inayopita wakati wake bila ya udhuru unaokubalika ki Shariy’ah.

 

 

[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy Lima’aaliy Shaykh Swaalih bin Fawzaan]

 

 

Share