Al-Lajnah Ad-Daaimah: Hajj: Hukmu Ya Kumuita Mtu Aliyetoka Kuhiji Jina La “Haji”
Hukmu Ya Kumuita Mtu Aliyetoka Kuhiji Jina La “Haji”
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Ni ipi hukmu ya kuita baadhi ya watu “Haji”?
JIBU:
Ama kumuita yule aliyehiji kwa jina la “Haji”, ni bora kuepuka hilo.
Kwani kutekeleza mambo ya waajib kishariy’ah hakutoi (kumpa mtu) majina na lakabu bali kunapatikana thawabu kutoka kwa Allaah Ta’aalaa kwa aliyetakabaliwa (matendo yake).
Na inampasa Muislamu asijihusishe na mfano wa mambo kama haya (ya kujipachika majina au kukubali kupachikwa majina kwa matendo ya ‘ibaadah anayoyafanya) ili iwe niyyah yake imetakasika kwa ajili ya wajihi wa Allaah Ta’aalaa.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah, 1/21718]