Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hajj: Hukmu Ya Kujiita Au Kuitwa “Haji Fulani”

 

Hukmu Ya Kujiita Au Kuitwa “Haji Fulani”

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Katika nchi nyingi za Kiislamu punde tu baada ya Mahujaji kurejea kutoka katika Ardhi Takatifu baada ya kutekeleza fardhi (ya Hajj) anapachikwa lakabu ya “Haji” yule aliyetekeleza fardhi na linabaki (lakabu) hilo likilazimiana nae daima; ni nini hukmu ya hilo?

 

 

JIBU:

 

Hilo ni kosa. Kwani ndani yake kuna aina fulani ya Riyaa.

Asijipe lakabu hiyo (kujiita “Haji”), na wala haipasi watu kumuita kwa lakabu hiyo; kwa sababu watu wakati wa zama za Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hawakuwa wakisema kwa aliyehiji kuwa wewe ni “Haji”.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa War-Rasaaail, 24/204]

 

Share