Skip to main content

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Tafsiyr Gani Anatakiwa Awe Nayo Mtafutaji Elimu?

 Tafsiyr Gani Anatakiwa Awe Nayo Mtafutaji Elimu?

Imaam Muhammad bin Swaalih Al-‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

Alhidaaya.com

SWALI:

Allaah Awahifadhi na Azinyooshe hatua zenu, Twaalib Al-‘Ilm (Mwanafunzi, Mtafutaji elimu) anataka kusoma Tafsiyr, ni zipi Tafsiyr mashuhuri ambazo anahitaji kuwa nazo mwanafunzi?

JIBU:

Maona amiliki Tafsiyr ya Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah), na Tafsiyr ya Shaykh wetu ‘Abdur-Rahmaan As-Sa’diy, kwani hizo mbili ni Tafsiyr bora nilizozipitia katika vitabu vya Tafsiyr.

Vilevile kuna Tafsiyr zingine kwa mtafutaji elimu mwenye shauku na kutaka (kusoma), kama vile Tafsiyr ya Al-Qurtwubiy na Tafsiyr Ash-Shawkaaniy. Na’am.

[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy li-Fadhwiylah Ash-Shaykh Al-'Allaamah Muhammad bin Swaalih Al-'Uthaymiyn]

N.B. Katika sehemu nyingine, Imaam Ibn ‘Uthaymiyn vilevile aliitaja Tafsiyr ya Ibn Jariyr Atw-Twabariy kuwa ni katika Tafsiyr bora ila inahitaji mwenye maarifa kutokana na upana wa ufafanuzi wake na wingi wa maelezo ya wapokezi wa Ahaadiyth, Athaar na Isnaad.