Taraawiyh: Uzushi Wa Adhkaar Kila Baada Ya Rakaa Mbili Au Nne Za Taraawiyh

 

 

Uzushi Wa Adhkaar Kila Baada Ya Rakaa Mbili Au Nne Za Swalaah Ya Taraawiyh  

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

assalam aleikum. amma baad nina maswala machache kuhusu ramadhan na yalyomo ndani yake.

je kunao adhkar ambazo mtume Salla-Allah alayhi wa sallam alizileta baada ya kila rakaa mbili za taraweeeh kama ifuatayo?

Ashadu anlaaillaha ila allah nastaghfiru allah nasalukajannatu wanaudhubika minanari. mara3 allahumakaghafdur tuhibulafwaa faafuanna mara 3......hii nyiradi nina isikia katika kila kipindi cha swala watu wakileta kwa sauti.je ina juzu?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hakuna dalili kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  au Maswahaba walikuwa akileta adhkaar yoyote kila baada ya Rakaa mbili katika Swalaah ya Taraawiyh. Kwa hiyo hayo ni mafunzo yaliyo kinyume na mafunzo sahihi ya Sunnah na hivyo ni bid’ah. 

 

Bid'ah hii inaokenana ikifanyika katika Swalaah ya Taraawiyh zaidi katika kila baada ya Rakaa nne. Na baadhi ya Misikiti huweka hata mabango yaliyoandikwa Tasbiyh ya kusoma katika mapumziko hayo. Hivyo inatupasa tuepukane na Bid'ah kama hizo na tufuate mafunzo sahihi ya Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Adhkaar zilizothibiti ni ambazo unatakiwa useme mwisho kabisa wa kumaliza Swalaah yako ya Qiyaamul-Layl nayo ni: 

سُـبْحانَ المَلِكِ القُدّوس

Subhaanal-Malikul-Qudduus

“Ametakasika Mfalme Mtakatifu"

 

(mara tatu na mara ya mwisho unavuta kwa sauti na kusema)

 رب الملائكةِ والرّوح

 

“Rabb wa Malaika na wa Jibriyl”

 

Bonyeza hapa upate maelezo zaidi:

 

033-Hiswnul-Muslim: Du’aa Baada Ya Salaam Katika Swalaah Ya Witr

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

 

  

Share