111-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Masad: تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ

 

 

Sababu Za Kuteremshwa

(Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Suwrah Al-Masad

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

111-Suwratul-Masad:

 

تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ ﴿١﴾

1. Imeteketea mikono miwili ya Abuu Lahab na ameteketea.

 

مَا أَغْنَىٰ عَنْهُ مَالُهُ وَمَا كَسَبَ ﴿٢﴾

2. Haikumfaa mali yake na yale aliyoyachuma.

 

سَيَصْلَىٰ نَارًا ذَاتَ لَهَبٍ ﴿٣﴾

3. Ataingia na kuungua moto wenye mwako.

 

وَامْرَأَتُهُ حَمَّالَةَ الْحَطَبِ ﴿٤﴾

4. Na mke wake mbebaji kuni za moto.

 

فِي جِيدِهَا حَبْلٌ مِّن مَّسَدٍ ﴿٥﴾

5. Katika shingo yake kamba ya mtende iliyosokotwa madhubuti.

 

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ـ قَالَ: لَمَّا نَزَلَتْ: ((‏وَأَنْذِرْ عَشِيرَتَكَ الأَقْرَبِينَ)) صَعِدَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَى الصَّفَا فَجَعَلَ يُنَادِي:  ((يَا بَنِي فِهْرٍ، يَا بَنِي عَدِيٍّ))‏‏.‏ لِبُطُونِ قُرَيْشٍ حَتَّى اجْتَمَعُوا، فَجَعَلَ الرَّجُلُ إِذَا لَمْ يَسْتَطِعْ أَنْ يَخْرُجَ أَرْسَلَ رَسُولاً لِيَنْظُرَ مَا هُوَ، فَجَاءَ أَبُو لَهَبٍ وَقُرَيْشٌ فَقَالَ: ((أَرَأَيْتَكُمْ لَوْ أَخْبَرْتُكُمْ أَنَّ خَيْلاً بِالْوَادِي تُرِيدُ أَنْ تُغِيرَ عَلَيْكُمْ، أَكُنْتُمْ مُصَدِّقِيَّ))‏‏.‏ قَالُوا نَعَمْ، مَا جَرَّبْنَا عَلَيْكَ إِلاَّ صِدْقًا‏.‏ قَالَ: ((فَإِنِّي نَذِيرٌ لَكُمْ بَيْنَ يَدَىْ عَذَابٍ شَدِيدٍ)).‏ فَقَالَ أَبُو لَهَبٍ: "تَبًّا لَكَ سَائِرَ الْيَوْمِ، أَلِهَذَا جَمَعْتَنَا؟" فَنَزَلَتْ:  ‏((‏تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ * مَا أَغْنَى عَنْهُ مَالُهُ وَمَا كَسَبَ))

 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema, Pindi ilipoteremka: “Na onya (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) jamaa zako wa karibu”. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipanda juu ya mlima wa Asw-Swafaa akawa anaita na kulingania: “Enyi Baniy ‘Adiyy!” Kwa makabila na matumbo ya ki-Quraysh hadi yalipokusanyika na ikawa mtu siku hiyo ambayo hakuweza kutoka humtuma mtu ambaye atamuwakilisha ili ajue kuna nini. Abuu Lahab pamoja na ma-Quraysh wengine walifika na hapo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Lau nikiwajulisha kuwa kuna msafara kwenye bonde unakuja kuwashambulia; je, mtanisadiki?” Wakasema: “Ndio, hatukuwahi kujaribu kutoka kwako isipokuwa ni kweli tupu!” Hapo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika mimi ni mwonyaji kwenu, kabla ya kufikia adhabu kali)).  Abuu Lahab akasema:  “Ole wako siku nzima ya leo, ni kwa hili ndilo ulilotukusanyia?” Baada ya hapo ikateremka: “Imeteketea mikono miwili ya Abuu Lahab na ameteketea. Haikumfaa mali yake na yale aliyoyachuma…” [Al-Masad: 111] [Al-Bukhaariy, Kitaab At-Tafsiyr]

 

 

Pia,

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم خَرَجَ إِلَى الْبَطْحَاءِ فَصَعِدَ إِلَى الْجَبَلِ فَنَادَى :((يَا صَبَاحَاهْ))‏ فَاجْتَمَعَتْ إِلَيْهِ قُرَيْشٌ قَالُوا: مَا لَكَ؟  قَالَ: (( أَرَأَيْتُمْ لَوْ أَخْبَرْتُكُمْ أَنَّ الْعَدُوَّ يُصَبِّحُكُمْ أَوْ يُمَسِّيكُمْ أَمَا كُنْتُمْ تُصَدِّقُونِي)) ‏  قَالُوا: "بَلَى‏!" ‏ قَالَ: (( فَإِنِّي نَذِيرٌ لَكُمْ بَيْنَ يَدَىْ عَذَابٍ شَدِيدٍ)) ‏ فَقَالَ أَبُو لَهَبٍ: "تَبًّا لَكَ أَلِهَذَا جَمَعْتَنَا فَأَنْزَلَ اللَّهُ: ((‏تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ‏...)))

 

Amepokea Al-Bukhaariy kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka kwenda Al-Batw-haa akapanda juu ya jabali akaita kwa kusema: ((Ee, kumekucha!)) Wakakusanyika kwake Ma-Quraysh akasema: ((Je, mnaonaje iwapo nitawaeleza kwamba adui atawajieni asubuhi, au atawajieni jioni; je, mtakuwa ni wenye kunisadikisha?)) Wakasema; “Ndio” Akasema: ((Hakika mimi ni mwonyaji kwenu, kabla ya kufikia adhabu kali)) akasema Abuu Lahab: “Kwa ajili ya hili umetukusanya? Kuangamia ni kwako!” Allaah Akateremsha: “Imeteketea mikono miwili ya Abuu Lahab na ameteketea…”

 

Mpaka mwisho wa Suwrah (Taz. Fat-h Al-Baariy) na katika mapokezi mengine, akasimama na hali anaipukusa mikono yake na huku anasema, “Maangamivu ni yako siku zote, ni kwa ajili ya hili umetukusanya?” Allaah Akateremsha: “Imeteketea mikono miwili ya Abuu Lahab na ameteketea…”

 

Rejea pia:

 

026-Asbaabun-Nuzuwl:Ash-Shu'araa Aayah 214: وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ 

 

 

Share