Shaykh Fawzaan: Sha'baan: Je Laylatul-Qadr Inatokea Katika Nisfwu Sha'baan?
Je, Laylatul-Qadr Inatokea Katika Nisfwu Sha'baan?
Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Je, Laylatul-Qadr inakuwa tarehe 15 Sha'baan?
JIBU:
Hapakuthibiti fadhila yoyote katika usiku wa Niswfu Sha´baan inayotofautiana na masiku wala usiku wowote wa mwezi wa Sha´baan. Hapakuthibiti lolote katika hili.
Vilevile wanasema kuwa Laylatul-Qadr inakuwa katika usiku wa Niswfu Sha´baan, si kweli. Laylatul-Qadr inakuwa katika Ramadhwaan. Kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amesema:
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ ﴿١﴾
1. Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatil-Qadr (usiku wa Qadar). [Al-Qadr: 01]
Laylatul-Qadr inakuwa katika masiku kumi ya mwisho ya Ramadhwaan. Hili ni kwa Ijmaa´. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaitafuta katika Ramadhwaan na hakuwa anaitafuta katika mwezi wa Sha´baan.
Wapi wametoa haya kwamba Laylatul-Qadr inakuwa katika usiku wa Niswfu Sha´baan?