Keki Za Banoffee Za Vikombe

 

Keki Za Banoffee Za Vikombe

 

 

Vipimo Vya Keki

 

Vinatoa vikeki 12

 

Siagi – 140 gm

Sukari ya brown ya rangi isiyokoza (light) – 200 gm

Mayai  - 3

Unga – 300 gm

Baking powder -  ½ kijiko cha chai

Bicarbonate soda – ½ kijiko cha chai

Ndizi saizi ndogo – 3  

Mdalasini – 1 kijiko cha chai

Mtindi – 4 vijiko vya kulia

Jozi (walnuts) zilokatwakatwa – 50 gm

 

 

 

Vipimo Vya Icing Sugar

 

 

Sukari  ya brown – 200 gm

Siagi – 100 gm

Maziwa au malai (cream) – vijiko 8 vya kulia

Icing sugar – 400 gm

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Keki  

 

  1. Washa oveni moto wa 180°C
  2. Saga siagi na sukari mpaka iwe nyororo na laini. Tumia machine ukiwa unayo. Vunja yai moja moja huku unachanganya vizuri kwa speed ndogo.
  3. Ponda ndizi kwa uma kisha changanya katika mchanganyiko wa keki na changanya pamoja na mtindi.
  4. Tia unga kidogo kidogo pamoja na mdalasini, bicarbonate soda, baking powder na uchanganye pole pole. Tia jozi (walnuts), uchanganye.
  5. Gawanya mchanganyiko katika karatasi za vikombe vya keki au vibakuli vya  kupikia keki ujaze kila moja ifikie 3/4 .
  6. Choma (bake) kwa muda wa dakika 20 mpaka keki zipande juu na ziwive na zigeuke rangi ya hudhurungi.
  7. Hakikisha kuwiva kwake kwa kuchomeka kijiti cha mishkaki pindi kikitoka bila ya kunata basi keki zimewiva.
  8. Epua uache zipowe.

 

Namna Ya Kutayarisha Icing Sugar

 

  1. Weka siagi na sukari ya brown katika sufuria au kikaangio uache iyayuke itoe kama povupovu na sukari kuyayuka.
  2. Epua katika moto tia cream na icing sugar na changanya vizuri.
  3. Acha ipowe ili iwe ya kumiminika vizuri katika kibomba cha icing. (piping consistency).
  4. Mimina katika kibomba cha icing na upambe juu ya keki wakati ingali bado dafudafu (warm)
  5. Pambia vipande vya ndizi kavu, (banana chips), vipande vya tofi, au vipande vya chokoleti.

 

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

Share