08-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Kuingia Hijr Ismaa'iyl Katika Kufanya Twawaaf

 

Kuingia Hijr Ismaa'iyl Katika Kufanya Twawaaf

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

   

 

SWALI:

 

Je, inaruhusiwa kuingia katika Hijr Ismaa'iyl (chumba cha Ismaa’iyl) wakati wa kufanya twawaaf?

 

 

JIBU:

 

Hairuhusiwi kuingia Hijr Ismaa'iyl wakati wa kufanya twawaaf katika Nyumba (Ka'abah) ikiwa ni kwa ajili ya Hajj au 'Umrah. Anayefanya hivyo hatopata thawabu kwa sababu twawaaf ni kuzunguka Ka'bah yote, na Hijr Ismaa'iyl ni sehemu ya Ka'bah. Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Anasema:

  

  وَلْيَطَّوَّفُوا بِالْبَيْتِ الْعَتِيقِ ﴿٢٩﴾

...na watufu kwenye Nyumba ya Kale. (Al-Ka’bah).  [Al-Hajj: 29]

 

 

Na kutoka kwa Mama Wa Waumini 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) ambaye amesema: "Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu Hijr akasema: ((Ni sehemu ya Nyumba [Ka'bah] [Muslim na wengineo]

 

 

Na Riwaayah nyengine amesema pia: "Niliapa kuswali ndani ya Nyumba naye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akasema: ((Swali katika Hijr kwani hakika Hijr ni sehemu ya Nyumba …. )) 

 

 

 Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

[Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah lil-Buhuwth al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. Mjalada 11, Uk. 233, Swali Namba 1, Fatwa Namba 1775 - Fataawa al-Hajj wal-'Umrah waz-Ziyaarah – Uk. 77

-Imejumuisha:

 

Kiongozi Mkuu: Shaykh 'Abdul 'Aziyz bin 'Abdillaah bin Baaz

 

Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdur-Razzaaq 'Afiyfiy

 

Mjumbe: Shaykh 'Abdullaah bin Ghudayyaan

 

Mjumbe: Shaykh 'Abdullah bin Qu'uwd]

 

 

 

Share