Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hajj: Masharti Ya Udhwhiyah Ni Yepi?
Masharti Ya Udhwhiyah Ni Yepi?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Ni yepi masharti ya Udhwhiyah (Kuchinja kwa ajili ya 'Iyd Al-Adhw-haa)?
JIBU:
1-Awe mnyama wa mifugo nao ni ngamia, ng’ombe na kondoo (au mbuzi).
2-Afikie umri unaokubalika ki-Shariy’ah:
- Kondoo miezi sita
- Mbuzi mwaka mmoja
- Ng’ombe miaka miwili
- Ngamia miaka tano
3-Asiwe mnyama mwenye kasoro yoyote ile katika mwili wake kama vile:
- Asiwe mwenye jicho lenye ubovu (chongo, jeupe weupe wa upofu) lenye kudhihirika.
- Asiwe mgonjwa mwenye kudhihirika ugonjwa wake.
- Asiwe kilema mwenye kudhihirika kilema chake (akawa anashindwa kutembea kawaida).
- Asiwe aliyedhoofika, gofu, asiyechaguliwa (asiyetakiwa).
[Majmuw’ Al-Fataawaa (12/25)]