Ukumbusho Wa Kuzuia Kukata Kucha Na Nywele Kwa Anayenuia Kuchinja
Ukumbusho Wa Kuzuia Kukata Kucha Na Nywele Kwa Anayetaka Kuchinja
Tunapenda kuwakumbusha ndugu zetu wengi jambo ambalo wanaghafilika nalo, kuwa, wenye kunuia kuchinja au kuchinjiwa (anayewakilisha mtu kumchinjia), kuanzia unapoandama tu mwezi wa Dhul-Hijjah wanatakiwa wajizuie kukata nywele za mwili na kukata kucha mpaka watakapomaliza kuchinja. Haya ni maamrisho yanayopatikana katika Hadiyth ifuatayo:
عن أم سلمة رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إِذَا رَأَيْتُمْ هِلَالَ ذِي الْحِجَّةِ وَأَرَادَ أَحَدُكُمْ أَنْ يُضَحِّيَ ، فَلْيُمْسِكْ عَنْ شَعْرِهِ وَأَظْفَارِهِ )) وفي رواية: ((فَلا يَمَسَّ مِنْ شَعَرِهِ وَبَشَرِهِ شَيْئًا))
Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukiandama mwezi wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake)) na katika riwaaya nyengine ya Muslim (1977); ((basi asitoe kitu katika nywele zake wala ngozi yake)) [Muslim]
Faida na mafunzo ziyada yafuatayo:
Kuchinja - Fadhila, Hikmah Na Hukmu Zake
Al-Lajnah Ad-Daaimah: Anayetia Niyyah Kuchinja Asikate Au Kunyoa Nywele Au Kukata Kucha
Al-Lajnah Ad-Daaimah: Nani Wa Kujizuia Kukata Nywele Na Kucha Katika Kuchinja (Udhwhiyah)?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Udhwhiyah (Kuchinja) Ni Sunnah Iliyosisitizwa Kwa Mwenye Uwezo
Imaam Ibn Baaz - Vipi Kuigawa Nyama Ya Udhw-hiyah
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kuigawa Nyama Ya Udhw-hiyah Kama Zawadi Au Swadaqah Iwe Freshi Si Ya Kupikwa
Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Masharti Ya Udhwhiyah Ni Yepi?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Haijuzu Kumpa Mchinjaji Wa Udhw-hiyah Nyama Kama Ujira Wake
Imaam Ibn Baaz - Hukmu Ya Kuchinja Kwa Kutumia Mkono Wa Kushoto