Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Maulidi: Yangelikuwa Maulidi Ni Ukamilifu Wa Dini Yangekuweko Kabla Kufariki Nabiy ﷺ

 

Yangelikuwa Maulidi Ni Katika Ukamilifu Wa Dini Yangekuweko Kabla Ya Kufariki Kwa Nabiy  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymin (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Yangelikuwa Mawlid ni katika ukamilifu wa Dini, basi yangelikuweko kabla ya kufariki kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Lakini kwa vile si katika ukamilifu wa Dini basi hakika hayawezi kuwa ni katika mambo ya Dini kwa sababu Allaah (Ta’aalaa) Anasema:

 الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ...

Leo Nimekukamilishieni Dini yenu...  [Al-Maaidah: 3]

 

Na ambaye anadai kuwa ni katika ukamilifu wa Dini ilhali yamezuka baada ya kufariki kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), basi kauli yake inakusanya kukadhibisha Aayah hiyo tukufu. Kwa hiyo kusherehekea Mawlid ni bid’ah na ni haramu.

 

Kisha tunasikia kuwa katika hizo sherehe za Mawlid kuna munkaraat (maovu) makubwa ambayo hayakubaliki kiakili wala ki-shariy’ah kama kuimba qaswiydah za kuvuka mipaka katika kumtukuza na kumsifu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hadi kwamba wamempandisha kuwa ni mkubwa (mtukufu) kuliko Allaah ('Azza wa Jalla). Tunajikinga kwa Allaah.

 

 

[Majmuw’ Fataawaa Ibn ‘Uthaymiyn (2/350)]

 

 

Share