Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kutamka Niyyah Katika ‘Ibaadah Ni Bid’ah Bali Mahali Pake Ni Moyoni
Kutamka Niyyah Katika ‘Ibaadah Ni Bid’ah Bali Mahali Pake Ni Moyoni
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
“Kutamka Niyyah katika ‘ibaadah zote ni bid’ah. Hivyo haijuzu mtu kusema katika kutia wudhuu: “Nawaytu an atawadhw-dhwaa (natia niyyah kutawadha).” Wala katika kuswali “Nawaytu an uswalliy (natia niyyah kuswali).” Wala katika kutoa sadaka “Nawaytu an ataswaddaq (natia niyyah kutoa sadaka).” Wala katika Swawm “Nawaytu an aswuwma (natia niyyah kufunga).” Wala katika Hajj “Nawaytu an ahujja (natia niyyah kuhiji).”
Kwa hivyo, kutamka niyyah katika ‘ibaadah zote haikuthibiti kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Huenda mtu akasema: “Nafanya hivi kwa ajili ya ikhlaasw li-LLaah (kumtakasia niyyah Allaah).” Basi tunasema: “Ikhlaasw pia mahali pake ni moyoni, na chochote ambacho mahali ni moyoni, basi inatosheleza niyyah moyoni.”
[Silsilatu Fataaawaa Nuwr ‘Alad-Darb, Kanda (349)]