04-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Waliymah (Karamu Ya Harusi)

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلنِّكَاحِ

Kitabu cha Nikaah (Ndoa)

 

بَابُ اَلْوَلِيمَةِ

04-Mlango Wa Waliymah (Karamu Ya Harusi)

 

 

 

 

 

890.

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  رَأَى عَلَى عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ بْنِ عَوْفٍ أَثَرَ صُفْرَةٍ، قَالَ: {" مَا هَذَا؟ "، قَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنِّي تَزَوَّجْتُ اِمْرَأَةً عَلَى وَزْنِ نَوَاةٍ مِنْ ذَهَبٍ. فَقَالَ: " فَبَارَكَ اَللَّهُ لَكَ، أَوْلِمْ وَلَوْ بِشَاةٍ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ 

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Alimuona ‘Abdir-Rahmaan bin ‘Awf ana athari ya manukato ya zafarani, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Una jambo gani? Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Nimeoa mwanamke (fulani) kwa uzito wa kokwa ya dhahabu.[1] Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Allaah Akubarikie. Fanya waliymah (karamu) japo mbuzi.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

 

 

891.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ   {إِذَا دُعِيَ أَحَدُكُمْ إِلَى اَلْوَلِيمَةِ فَلْيَأْتِهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

وَلِمُسْلِمٍ:{إِذَا دَعَا أَحَدُكُمْ أَخَاهُ، فَلْيُجِبْ، عُرْسًا كَانَ أَوْ نَحْوَهُ}

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anapoalikwa mmoja wenu katika waliymah (karamu) aende.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

Na katika Riwaayah ya Muslim inasema: “Mmoja wenu anapomualika nduguye ajibu (aende) iwe ni harusi au mfano wake.”[2]  

 

 

 

892.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {شَرُّ اَلطَّعَامِ طَعَامُ اَلْوَلِيمَةِ: يُمْنَعُهَا مَنْ يَأْتِيهَا، وَيُدْعَى إِلَيْهَا مَنْ يَأْبَاهَا، وَمَنْ لَمْ يُجِبِ اَلدَّعْوَةَ فَقَدْ عَصَى اَللَّهَ وَرَسُولَهُ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Chakula kibaya ni chakula cha waliymah (karamu ya harusi) kinanyimwa anayekiendea na hualikwa anayekikataa. Na asiyejibu mualiko atakuwa amemuasi Allaah na Rasuli wake.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

893.

وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {إِذَا دُعِيَ أَحَدُكُمْ فَلْيُجِبْ، فَإِنْ كَانَ صَائِمًا فَلْيُصَلِّ، وَإِنْ كَانَ مُفْطِرًا فَلْيُطْعَمْ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ أَيْضًا 

وَلَهُ مِنْ حَدِيثِ جَابِرٍ نَحْوُهُ. وَقَالَ:{فَإِنْ شَاءَ طَعِمَ وَإِنْ شَاءَ تَرَكَ}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anapoalikwa mmoja wenu aitike, akiwa ana swawm aombe du’aa na akiwa hana swawm basi ale.” [Imetolewa na Muslim]

Vile vile Muslim amepokea kutoka katika Hadiyth ya Jaabir kama hiyo na akasema: “Akipenda atakula na akipenda ataacha” 

 

 

 

894.

وَعَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ   {طَعَامُ الْوَلِيمَةِ أَوَّلَ يَوْمٍ حَقٌّ، وَطَعَامُ يَوْمِ اَلثَّانِي سُنَّةٌ، وَطَعَامُ يَوْمِ اَلثَّالِثِ سُمْعَةٌ، وِمَنْ سَمَّعَ سَمَّعَ اللهُ بِهِ} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَاسْتَغْرَبَهُ، وَرِجَالُهُ رِجَالُ اَلصَّحِيحِ

وَلَهُ شَاهِدٌ: عَنْ أَنَسٍ عِنْدَ اِبْنِ مَاجَهْ

Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Chakula cha waliymah (karamu) siku ya kwanza ni haki, chakula cha siku ya pili ni Sunnah, na chakula cha siku ya tatu ni riyaa. Mwenye kuidhihirisha amali yake kwa riyaa Allaah Atamfedhehesha Siku ya Qiyaamah.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy]

 

 

 

895.

وَعَنْ صَفِيَّةَ بِنْتِ شَيْبَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ:{أَوْلَمَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  عَلَى بَعْضِ نِسَائِهِ بِمُدَّيْنِ مِنْ شَعِيرٍ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Swafiyyah bint Shaybah[3] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alifanya waliymah (karamu) alipomuowa mmoja katika wakeze kwa pishi mbili za shayiri.”[4] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

896.

وَعَنْ أَنَسٍ قَالَ: {أَقَامَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  بَيْنَ خَيْبَرَ وَالْمَدِينَةِ ثَلَاثَ لَيَالٍ، يُبْنَى عَلَيْهِ بِصَفِيَّةَ، فَدَعَوْتُ اَلْمُسْلِمِينَ إِلَى وَلِيمَتِهِ، فَمَا كَانَ فِيهَا مِنْ خُبْزٍ وَلَا لَحْمٍ، وَمَا كَانَ فِيهَا إِلَّا أَنْ أَمَرَ بِالْأَنْطَاعِ، فَبُسِطَتْ، فَأُلْقِيَ عَلَيْهَا اَلتَّمْرُ، وَالْأَقِطُ، وَالسَّمْنُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ

Kutoka kwa Anas amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikaa siku tatu baina ya Khaybar na Madiynah akimkamilishia Swafiyyah ndoa yake. Nikawaalika Waislamu katika waliymah (karamu) yake, hakukuwa na mkate wala nyama. Akaamrisha iletwe busati la ngozi likatandikwa ikawekwa juu yake tende, aqitw[5] na samli.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

 

 

897.

وَعَنْ رَجُلٍ مِنْ أَصْحَابِ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ:{إِذَا اِجْتَمَعَ دَاعِيَانِ، فَأَجِبْ أَقْرَبَهُمَا بَابًا، فَإِنْ سَبَقَ أَحَدُهُمَا فَأَجِبِ اَلَّذِي سَبَقَ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَسَنَدُهُ ضَعِيفٌ

Kutoka kwa mtu mmoja katika Maswahaba amehadithia kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Wanapojumuika waalikaji wawili nenda kwa yule ambaye mlango wake uko karibu zaidi (nawe), mmoja kati yao atakapotangulia (kukualika) nenda kwa yule aliyetangulia.”[6] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na Isnaad yake ni dhaifu] 

 

 

 

898.

وَعَنْ أَبِي جُحَيْفَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَا آكُلُ مُتَّكِئًا} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Abuu Juhayfah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mimi sili nikiwa nimeegemea.”[7] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

899.

وَعَنْ عُمَرَ بْنِ أَبِي سَلَمَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {يَا غُلَامُ! سَمِّ اَللَّهَ، وَكُلْ بِيَمِينِكَ، وَكُلْ مِمَّا يَلِيكَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Umar bin Abuu Salamah[8] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ee kijana! Mtaje Allaah, na kula kwa mkono wako wa kuume, na kula kinachokuelekea.” [Al-Bukhaariy, Muslim] 

 

 

 

900.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  أُتِيَ بِقَصْعَةٍ مِنْ ثَرِيدٍ، فَقَالَ: "كُلُوا مِنْ جَوَانِبِهَا، وَلَا تَأْكُلُوا مِنْ وَسَطِهَا، فَإِنَّ اَلْبَرَكَةَ تَنْزِلُ فِي وَسَطِهَا} رَوَاهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَهَذَا لَفْظُ النَّسَائِيِّ، وَسَنَدُهُ صَحِيحٌ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliletewa sahani ya thariyd[9] akasema: kuleni kando yake wala msile katikati yake, kwa hakika Baraka huteremka kati kati yake“ [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na tamshi hili ni la An-Nisaaiy na Isnaad yake ni Swahiyh]

 

 

 

901.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: {مَا عَابَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  طَعَامًا قَطُّ، كَانَ إِذَا اِشْتَهَى شَيْئًا أَكَلَهُ، وَإِنْ كَرِهَهُ تَرَكَهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hajapatapo kamwe hakukiaibisha chakula, alikuwa akitamani kitu hula na asipokipenda hukiacha.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

902.

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، عَنْ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {لَا تَأْكُلُوا بِالشِّمَالِ، فَإِنَّ اَلشَّيْطَانَ يَأْكُلُ بِالشِّمَالِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msile kwa kushoto, hakika shaytwaan hula kwa kushoto.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

903.

وَعَنْ أَبِي قَتَادَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {إِذَا شَرِبَ أَحَدُكُمْ، فَلَا يَتَنَفَّسْ فِي اَلْإِنَاءِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَلِأَبِي دَاوُدَ: عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ نَحْوُهُ، وَزَادَ: {أَوْ يَنْفُخْ فِيهِ} وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ

Kutoka kwa Abuu Qataadah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Yeyote kati yenu anapokunywa asipumue ndani ya chombo.”[10] [Al-Bukhaariy, Muslim]

Na Abuu Daawuwd amepokea Riwaayah kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Abbaas Hadiyth kama hii na akaongezea: “…wala asipumulie humo.” [Na ameisahihisha At-Tirmidhiy]

 

 

[1] Nawaah ya dhahabu ni takribani gramu 18.4 za dhahabu

[2] Kujibu mwito wa sherehe ya harusi au jambo lingine ni wajibu, isipokuwa kuwe kuna yenye kuchukiza, hapo haifai kwenda. Na iwapo atenda na akaona chukizo hilo anawajibika kuukanya, wasipokatazika wanapaswa waondoke.

[3] Huyu ni Swafiyyah bint Shaybah bin ‘Uthmaan bin Abiy Twalhah Al-‘Abadariy wa ukoo wa Banuu ‘Abdid-Daar. Inasemekana kuwa alimuona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) wakati wengine wanakataa hilo. Ibn Sa’d anakiri kuwa alikuwa Taabi’iy

 

[4] Shayiri nafaka inayofanana na ngano inayotumika kuwa chakula

 

[5] Aqitw ni maziwa yaliyogandishwa kwa moto

[6] Hadiyth hii ni dalili kuwa mtu anapoalikwa na watu wawili kwa pamoja basi aliye na haki ya kujibiwa ni yule aliyetangulia, wakilingana katika hilo atatangulizwa jirani. Na majirani wako kwa daraja, mwenye haki zaidi ni yule ambaye mlango wake uko karibu zaidi na mlango wako, wakilingana kwa hilo itapigwa kura.

[7] Al-Khatwabi amesema: “Makusudio ya ‘kuegemea’ katika Hadiyth hii ni kuketi juu ya tandiko laini kama yule aliyekusudia kula sana bali alikuwa akiketi bila kujituliza (ili asile sana) na huwa akila kidogo.” Wengine wamesema kuwa ‘kuegemea’ ni mtu kula kwa kuegemea kwa ubavu wake.

 

[8] ‘Umar bin Abiy Salamah ‘Abdillaah bin ‘Abdil-Asad bin Hilaal Al-Makhzuwm, alikuwa ni mtoto wa Ummul-Muuminiyna Ummu Salamah. Alizaliwa katika nchi ya Uhabeshi (Ethiopia) baina ya Hijrah ya Uhabeshi na ile ya Madiynah. Alifariki katika mji wa Madiynah mwaka 83 Hijriyyah.

[9]Thariyd’, ni mikate mepesi mikavu inayopikwa kwa unga wa shayiri (talbiynah/barley) na inakatwakatwa na kuchanganywa na supu ya nyama au mchuzi.  Inasemekana ni chakula tokea zama za Nabiy Ibraahiym ('Alayhis-Salaam) mpaka zama za Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Ni chakula waliokuwa wakikaribishwa Hujaji wa Makkah kabla ya Uislamu.

[10] Hii ina maana ni pale anapokunywa mtu asipumulie kwenye chombo, kwani ni sababu ya kueneza magonjwa.

Share