05-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Kugawa (Zamu)

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلنِّكَاحِ

Kitabu cha Nikaah (Ndoa)

 

بَابُ اَلْقَسْمِ

05-Mlango Wa Kugawa (Zamu)

 

 

 

 

904.

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  يَقْسِمُ، فَيَعْدِلُ، وَيَقُولُ: "اَللَّهُمَّ هَذَا قَسْمِي فِيمَا أَمْلِكُ، فَلَا تَلُمْنِي فِيمَا تَمْلِكُ وَلَا أَمْلِكُ} رَوَاهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ وَالْحَاكِمُ، وَلَكِنْ رَجَّحَ اَلتِّرْمِذِيُّ إِرْسَالَه

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akigawa muda baina ya wakeze, na akifanya uadilifu na anasema: Ee Allaah! Huu ni mgao wangu[1] katika ninachokimiliki, usinilaumu kwa kile unachomiliki nami sikimiliki.” [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na akaisahihisa Ibn Hibbaan na Al-Haakim, lakini At-Tirmidhiy ametilia nguvu kuwa ni Mursal]

 

 

 

905.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  عَنْ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {مَنْ كَانَتْ لَهُ اِمْرَأَتَانِ، فَمَالَ إِلَى إِحْدَاهُمَا، جَاءَ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ وَشِقُّهُ مَائِلٌ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ، وَسَنَدُهُ صَحِيح

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye wake wawili, na akaegemea zaidi kwa mmojawapo,[2] Siku ya Qiyaamah atakuja ilhali ubavu wake mmoja umeinama.” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na Isnaad yake ni sahihi]

 

 

 

906.

وَعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ:{مِنَ اَلسُّنَّةِ إِذَا تَزَوَّجَ اَلرَّجُلُ اَلْبِكْرَ عَلَى اَلثَّيِّبِ أَقَامَ عِنْدَهَا سَبْعًا، ثُمَّ قَسَمَ، وَإِذَا تَزَوَّجَ اَلثَّيِّبَ أَقَامَ عِنْدَهَا ثَلَاثًا، ثُمَّ قَسَمَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Katika Sunnah (mtu) anapooa mwanamwali juu ya mke mkuu akalale kwake siku saba kisha agawanye (siku). Na anapooa mke mkuu akae kwake siku tatu kisha agawanye (siku).” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

 

 

907.

وَعَنْ أُمِّ سَلَمَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  لَمَّا تَزَوَّجَهَا أَقَامَ عِنْدَهَا ثَلَاثًا، وَقَالَ: "إِنَّهُ لَيْسَ بِكِ عَلَى أَهْلِكِ هَوَانٌ، إِنْ شِئْتِ سَبَّعْتُ لَكِ، وَإِنْ سَبَّعْتُ لَكِ سَبَّعْتُ لِنِسَائِي} رَوَاهُ مُسْلِم

Kutoka kwa Ummu Salamah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipomuoa alikaa kwake siku tatu na akamuambia: Hutapata udhalilifu kwangu, nikipenda nitakukamilishia siku saba na iwapo nitakukamilishia siku saba vile vile nitawakamilishia wake zangu wote siku saba.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

908.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا {أَنَّ سَوْدَةَ بِنْتَ زَمْعَةَ وَهَبَتْ يَوْمَهَا لِعَائِشَةَ، وَكَانَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  يَقْسِمُ لِعَائِشَةَ يَوْمَهَا وَيَوْمَ سَوْدَةَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Sawdah bint Zam’ah aliitoa siku yake[3] kumpa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akimgawia ‘Aaishah siku yake na siku ya Sawdah.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

909.

وَعَنْ عُرْوَةَ قَالَ: {قَالَتْ عَائِشَةُ: يَا اِبْنَ أُخْتِي! كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  لَا يُفَضِّلُ بَعْضَنَا عَلَى بَعْضٍ فِي اَلْقَسْمِ مِنْ مُكْثِهِ عِنْدَنَا، وَكَانَ قَلَّ يَوْمٌ إِلَّا وَهُوَ يَطُوفُ عَلَيْنَا جَمِيعًا، فَيَدْنُو مِنْ كُلِّ اِمْرَأَةٍ مِنْ غَيْرِ مَسِيسٍ، حَتَّى يَبْلُغَ اَلَّتِي هُوَ يَوْمُهَا، فَيَبِيتَ عِنْدَهَا} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ وَاللَّفْظُ لَهُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ  

وَلِمُسْلِمٍ: عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  إِذَا صَلَّى اَلْعَصْرَ دَارَ عَلَى نِسَائِهِ، ثُمَّ يَدْنُو مِنْهُنَّ} اَلْحَدِيث

Kutoka kwa ‘Urwah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “’Aaishah aliniambia: Ee mpwa wangu! Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa hamfadhilishi yeyote miongoni mwetu katika mgawo wa kukaa kwake kwetu. Alikuwa akitutembelea sisi sote, akimkaribia kila mke bila ya kufanya jimai mpaka afike kwa yule ambaye ni siku yake[4] akalala kwake.” [Imetolewa na Ahmad na Abuu Daawuwd na matini ya Hadiyth ni yake, na akaisahihisha Al-Haakim]

Na katika Riwaayah ya Muslim kutoka kwa ‘Aaishah inasema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) anapomaliza kuswali alasiri akiwazungukia wakeze na akiwakaribia (kwa kuwabusu na kuwakumbatia)...” Mpaka mwisho wa Hadiyth

 

 

 

910.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  كَانَ يَسْأَلُ فِي مَرَضِهِ اَلَّذِي مَاتَ فِيهِ: " أَيْنَ أَنَا غَدًا ؟ "، يُرِيدُ: يَوْمَ عَائِشَةَ، فَأَذِنَ لَهُ أَزْوَاجُهُ يَكُونُ حَيْثُ شَاءَ، فَكَانَ فِي بَيْتِ عَائِشَةَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa katika maradhi yake aliyofia alikuwa akiuliza: “Kesho nitakuwa wapi?”[5] akikusudia siku ya ‘Aaishah. Wakeze wakamruhusu abaki pale anapopapenda. Akakaa katika nyumba ya ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا).” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

911.

وَعَنْهَا قَالَتْ:{كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  إِذَا أَرَادَ سَفَرًا أَقْرَعَ بَيْنَ نِسَائِهِ، فَأَيَّتُهُنَّ خَرَجَ سَهْمُهَا، خَرَجَ بِهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa anataka kusafiri hupiga kura baina ya wakeze, yoyote atakayepata kura husafiri pamoja naye.”[6] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

912.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ زَمْعَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَا يَجْلِدُ أَحَدُكُمْ اِمْرَأَتَهُ جَلْدَ اَلْعَبْدِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيّ

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Zam’ah[7] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu asimpige mkewe kipigo cha mtumwa.”[8] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

[1] Haikuwa muhimu kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuenda kwa wake zake kwa zamu, pamoja na kuwa alikuwa na mapenzi zaidi kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا), lakini aliendelea kufanya uadilifu kwa wake zake wengine. Kila mara alimuomba Allaah Amsamehe.

[2] Katika hali hii uadilifu hapa unakusudiwa ni ule wa vitu na kuwahudumia kwa usawa katika mahitaji mengine na kutoa zamu. Yote haya mtu ana uwezo wa kuyafanya au kutoyafanya, na haya ndio ataulizwa kama ameyafanyia uadilifu.  Kumpenda mtu na moyo kutekwa na mtu huyo si dhambi, maadamu halimzuii kufanya uadilifu.

[3] Hadiyth hii ina maana kwamba ikiwa mwanamke atakubaliwa mwenyewe kupunguziwa fedha zake za matumizi au zamu ya mumewe kwake, ni jambo linaloruhusiwa na mwanamme katika jambo hili si wa kulaumiwa, hata hivyo, ana haki ya kudai kurejeshewa haki yake wakati wowote.

[4] Hapa zamu inakusudiwa kulala kwake. Vinginevyo, mmoja anaweza kuruhusiwa kuongea na wengine na kuenda katika nyumba zao.

 

[5] Hii ina maana wakati wa ugonjwa wake, kuwepo kwa niyyah tu ya kubaki kwa mmoja sio tatizo. Hii ina maana ya ruhusa ya wake wengine, mtu anaweza kukaa kwa mmoja wao. Ugonjwa huu wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ulianzia kwa Maymwunah.

[6] Jina linalotokeza katika kura basi ndie wa kufuatana na Nabiy katika safari zake. Siku zote za safari hazihesabiwi katika zamu. Hata hivyo wake wanaweza kukubaliana wenyewe bila ya kuwepo kwa kura.

[7] Huyu ni ‘Abdullaah bin Zam’ah bin Al-Aswad bin ‘Abdil-Mutwalib bin Asad bin ‘Abdil-‘Uzza Al-Asadi, ni kaka wa Ummul Muuminiyna Sawdah bint Zam’ah. Alikuwa ni Swahaba mkubwa katika wakazi wa Madiynah. Aliuawa katika siku ya Ad-Daar.

 

[8] Ni haraam kumpiga mwanamke katika hali zozote isipokuwa moja tu la kufanya uzinifu. Haifai kumpiga usoni au kumpiga kiasi cha kumvunja, katika hali kama hiyo mume ataadhibiwa.

Share