09-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Al-Iylaa, Dhwihaar, Kafaara

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلنِّكَاحِ

Kitabu cha Nikaah (Ndoa)

 

 

بَابُ اَلْإِيلَاءِ وَالظِّهَارِ وَالْكَفَّارَةِ

09-Mlango Wa Al-Iylaa,[1] Dhwihaar[2], Kafaara[3]

 

 

 

 

929.

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {آلَى رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  مِنْ نِسَائِهِ وَحَرَّمَ، فَجَعَلَ اَلْحَرَامَ حَلَالًا، وَجَعَلَ لِلْيَمِينِ كَفَّارَةً} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَرُوَاتُهُ ثِقَاتٌ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliapa (kuwa hatawaingilia) wakeze kwa muda. Hivyo akajiharamishia (baadhi ya vitu) akafanya haraam kuwa halaal, na akafanya kafara kwa ajili ya kiapo.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na wapokezi wake ni madhubuti]

 

 

 

930.

وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ:{إِذَا مَضَتْ أَرْبَعَةُ أَشْهُرٍ وَقَفَ اَلْمُؤْلِي حَتَّى يُطَلِّقَ، وَلَا يَقَعُ عَلَيْهِ اَلطَّلَاقُ حَتَّى يُطَلِّقَ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيّ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Inapopita miezi minne muapaji atasimama ili atoe talaka, na talaka haipiti mpaka mume atoe talaka.”[4] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

931.

وَعَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {أَدْرَكْتُ بِضْعَةَ عَشَرَ مِنْ أَصْحَابِ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ كُلُّهُمْ يَقِفُونَ اَلْمُؤْلِي} رَوَاهُ اَلشَّافِعِيّ

Kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar[5] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nimewakuta zaidi ya Maswahaba kumi wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) wote wakimsimamisha aliyeapa.” [Imetolewa na Ash-Shafi’iyy]

 

 

 

932.

وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {كَانَ إِيلَاءُ اَلْجَاهِلِيَّةِ اَلسَّنَةَ وَالسَّنَتَيْنِ، فَوَقَّتَ اَللَّهُ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ، فَإِنْ كَانَ أَقَلَّ مِنْ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ، فَلَيْسَ بِإِيلَاءٍ} أَخْرَجَهُ اَلْبَيْهَقِيُّ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Ilikuwa kiapo cha Jahiliyyah[6] ni mwaka mmoja au miaka miwili, Allaah Akaweka muda wa miezi minne, inapokuwa ni uchache wa miezi minne hicho si kiapo.”[7] [Imetolewa na Al-Bayhaqiyy]

 

 

 

933.

وَعَنْهُ رَضِيَ اَللَّهُ تَعَالَى عَنْهُمَا، {أَنَّ رَجُلًا ظَاهَرَ مِنِ اِمْرَأَتِهِ، ثُمَّ وَقَعَ عَلَيْهَا، فَأَتَى اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  فَقَالَ: إِنِّي وَقَعْتُ عَلَيْهَا قَبْلَ أَنْ أُكَفِّرَ، قَالَ: "فَلَا تَقْرَبْهَا حَتَّى تَفْعَلَ مَا أَمَرَكَ اَللَّهُ"} رَوَاهُ اَلْأَرْبَعَةُ وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَرَجَّحَ النَّسَائِيُّ إِرْسَالَهُ  

وَرَوَاهُ اَلْبَزَّارُ: مِنْ وَجْهٍ آخَرَ، عَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ وَزَادَ فِيهِ:{كَفِّرْ وَلَا تَعُدْ} 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Mtu mmoja alimfanyia Dhwihaar mkewe kisha akamjamii, akamuendea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: “Mimi nimemjamii kabla ya kutoa kafara.” Akamuambia: “Usimkaribie mpaka utende Alilokuamrisha Allaah.” [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na akaisahihisha At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy amesema ni Mursal]

 

Al-Bazzaar ameipokea kwa njia nyingine kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) na akaongezea: “…toa kafara wala usirudie.”

 

 

 

934.

وَعَنْ سَلَمَةَ بْنِ صَخْرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {دَخَلَ رَمَضَانُ، فَخِفْتُ أَنْ أُصِيبَ اِمْرَأَتِي، فَظَاهَرْتُ مِنْهَا، فَانْكَشَفَ لِي مِنْهَا شَيْءٌ لَيْلَةً، فَوَقَعَتْ عَلَيْهَا، فَقَالَ لِي رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  "حَرِّرْ رَقَبَةً" قُلْتُ: مَا أَمْلِكُ إِلَّا رَقَبَتِي. قَالَ: "فَصُمْ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ"، قُلْتُ: وَهَلْ أَصَبْتُ اَلَّذِي أَصَبْتُ إِلَّا مِنْ اَلصِّيَامِ ؟ قَالَ: "أَطْعِمْ عِرْقًا مِنْ تَمْرٍ بَيْنَ سِتِّينَ مِسْكِينًا"} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ، وَابْنُ اَلْجَارُود

Kutoka kwa Salamah bin Swakhr[8] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Uliingia mwezi wa Ramadhwaan, nikahofia kumjamii mke wangu nikamfanyia Dhwihaar, usiku mmoja kitu kikanifunikia mwilini mwake, nikamjamii. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaniambia: “Acha mtumwa huru.” Nikamuambia: “Similiki ila shingo yangu”. Akaniambia: “Funga (Swiyaam) miezi miwili mfululizo.” Nikamuambia: “Yale yaliyonifikia ni kwa sababu ya Swiyaam.” Akaniambia: “Lisha maskini tende (vikapu) sitini.”[9] [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa An-Nasaaiy, na akaisahihisha Ibn Khuzaymah na Ibn Al-Jaaruwd]

 

[1] Al-Iylaa ni kiapo anachoapa mtu kuwa hatomuingilia mke wake; au kumuambia mke wake moja kwa moja kwa kuapa kwa Allaah kuwa hatomuingilia tena. Allaah Ameweka muda wa miezi mine ya kurudisha uhusiano baina ya mume na mke. Ni vizuri kurudisha uhusiano, kwa kutoa kafaara kwa kiapo kwa muda uliopangwa. Vinginevyo talaka itakuwa imeshatoka; au kulingana na ‘Ulamaa wengine, mtu atalazimishwa kumuacha mkewe au kurudisha uhusiano kama mwanzoni.

 

[2] Dhwihaar imetokana na neno Dhwahr kwa maana ya mgongo au nyuma, ni kumfananisha mke wa mtu na mgongo wa mama yake. Aina hii ya mazungumzo katika lugha ya kiarabu ina maana ya kuwa: “Wewe ni kama mama yangu na ni haraam kwa ndoa yangu au kukuoa au kukuingilia”. Kulingana na Istwilahi za kishariy’ah Adhw-Dhwihaar ni kumfananisha mke wa mtu na mama wa mtu na hivyo kumfanya kuwa ni haraam kwake. Jambo hili kishariy’ah halizingatiwi kuwa ni talaka lakini ni lazima mtu atoe kafaara kabla ya kumrudia mke wake. Kafaara yake ni kumuacha huru mtu mtumwa au kufunga Swiyaam siku sitini kwa mfululizo au kuwalisha maskini sitini. Ni wajibu kutekeleza moja ya adhabu hii.

 

[3] Kaffaarah ina maana ya kutubia kwa madhambi hayo mawili yaliyotajwa hapo juu.

[4] Katika hali ya kuapa mtu huulizwa aache au aendelee na mahusiano, nayo hufanyika baada ya miezi minne. Kama hataki kufanya hivyo, anaweza kutengua ndoa yake kwa msaada wa mtawala, na baada ya kumalizia eda yake ataruhusiwa kuolewa tena.

[5] Huyu ni Abuu Ayuwb Sulaymaan bin Yasaar, muachwa huru wa Ummul-Mu’miniyn Maymuwnah. Alikuwa ni mmoja wa ‘Ulamaa saba wakubwa wa Fiqhi na ni Taabi’ mkubwa katika mji wa Madiynah. Ni mtu madhubuti, mwenye taqwa na Mwanazuoni. Alifariki mwaka 107H akiwa na umri wa miaka 73.

 

[6] Wakati wa Ujahiliyah, mwanamke alionewa sana. Wakati mwingine kwa miaka, hajulikani yuko wapi si muolewa wala si aliyeachwa, yupo katikati. Vile vile haruhusiwi kuolewa baada ya kwisha Eda yake. Mwanamke alikuwa akionewa katika hili na kuachwa kwa muda wa miaka, nayo ilikuwa aina ya kumkomoa, ndipo Allaah Alipoweka miezi minne.

 

[7] Hadiyth hii inaweka wazi kuwa kama mahusiano yatarudi kabla ya miezi minne, basi itakuwa siyo Iylaa na hakutokuwepo na adhabu.

[8] Huyu ni Salamah bin Swakhr bin Sulaymaan Bin As-Samma Al-Bayadi anatokana na kizazi cha Banu Bayaad, ukoo wa Al-Khazraj, mmoja katika Al-Bukauwn miongoni mwa Swahaba.

 

[9] Araq moja ni pishi 15 (mfuko mmoja wa tende)

Share