Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Sha'baan: Hukmu Ya Kisimamo Cha Usiku Wa Niswf Sha’baan

 

Hukmu Ya Kisimamo Cha Usiku Wa Niswf Sha’baan

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah) amejibu kuhusu Swali la maudhui ya kisimamo cha usiku wa Niswf Sha’baan:

 

“Kisimamo cha usiku wa Niswf Sha’baan kiko katika hali au hukmu tatu:

 

1-Iwe ni ada (desturi) ya mtu kuwa anafanya hivyo (kuamka kwa ajili ya ‘ibaadah) kwa hiyo hufanya hata siku hiyo ya usiku wa Niswf Sha’baan kama anavyofanya nyusiku nyenginezo  bila ya kuufanya usiku huo kuwa ni makhsusi kwa kuzidisha ‘ibaadah. Jambo hili hakuna ubaya.

 

2- Kuswali  usiku wa Niswf Sha’baan juu ya kuwa hakuwa mtu akifanya hivyo katika nyusiko nyenginezo.  Hii ni bid’ah.

 

 

3-Kuswali usiku huo Swalaah zenye idadi maalumu, ambazo anakariri kila mwaka kuziswali.  Hii ni bid’ah shadidi (ya nguvu) zaidi kuliko ya hali ya pili na iko mbali zaidi na Sunnah.”

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/28-30)]

 

 

Share