Hapana uficho wowote kwa Muislamu ambaye moyo wake umesalimika na fikira zilizonyooka, kwamba utukufu wa elimu haupingwi, na yaliyopokelewa katika fadhila zake hiyo elimu, katu hayadhibitiki. Allaah (Subhaanahu Wataala) Anasema:
{{Je wanalingana wale wanaojua na wale wasiojua?}} [Az-Zumar: 9]