Saladi Ya Majani Na Mapilipili Mboga
VIPIMO
Saladi ya uwa (ya duwara) 1
Matango 2
Karoti 2
Pilipili kubwa la kijani tamu 1
Pilipili kubwa jekundu tamu 1
Nyanya 2
Limau au ndimu 1
NAMNA YA KUTAYARISHA
1. Katakata Saladi weka katika treya
2. Ukipenda kumenya tango, menya na kata vipande vya duara.
3. Kwaruza karoti na kata vipande vya duara au ukipenda kwaruza.
4. Katakata mapilipili kwa urefu
5. Kata nyanya kwanza nusu kisha katakata vipande vyembamba.
6. Changanya vizuri vitu vyote hivyo katika treya ya kupakulia na pambia kwa vipande vya limau au ndimu. Tayari kuliwa.