Ndizi Mbichi Za Nyama Ng'ombe-1
Ndizi Mbichi Za Nyama Ng'ombe-1
Vipimo
Ndizi mbichi - 10
Nyama - kilo 1
Nazi ya kopo - 1
Chumvi - 1 Kijiko cha chakula
Ndimu - 1
Bizari ya manjano - 1 Kijiko cha chai
Pili pili mbichi - 3
Nyanya (tomatoes) - 2
Kitunguu maji - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chakula
Namna ya Kutayarisha Na Kupika
- Kata nyama vipande vipande na uisafishe.
- Chemsha nyama weka chumvi, thomu, tangawizi na ndimu. Iache iwive.
- Kata kata nyanya na kitunguu, kisha mimina kwenye nyama inayochemka, weka na bizari nusu kijiko. Wacha supu iwive kisha weka pembeni. Ukumbusho: Hakikisha supu inakuwa kiasi na si nyingi.
- Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi.
- Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria.
- Weka maji ndani ya sufuria kisha zichemshe ndizi mpaka ziwe laini kidogo.
- Zimwage maji ndizi kisha mimina supu na nyama ndani ya ndizi.
- Mimina nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda.
- Weka pembeni zipoe.
- Pakua ndizi kwenye sahani au bakuli tayari kwa kuliwa.