Makaroni Ya Bashamella Na Nyama Ya Kusaga
Makaroni Ya Bashamella Na Nyama Ya Kusaga
Vipimo
Makoroni - 500 gms
Mafuta ya kuchemshia makoroni - ¼ kikombe
Nyama ya kusaga - ½ kilo
Mafuta - ¼ kikombe
Vitunguu vilivyokatwa (chopped) - 3
Tomato iliyokatwa ndogo ndogo - 1
Pilipili mboga iliyokatwa ndogo ndogo - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu
Pilipili manga - 1 kijiko cha supu
Chumvi - kiasi
Vipimo Vya Bashamela
Unga - 5 vijiko vya supu
Siagi - 3 vijiko vya supu
Maziwa - 5 vikombe
Jibini (Cheese) Ya Malai (Cream) - 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Makaroni
- Chemsha macaroni na mafuta hadi yawive mwaga maji na chuja.
Sosi Ya Nyama
- Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi.
- Tia thomu kaanga kidogo.
- Tia nyama, chumvi na pilipili kaanga hadi nyama iwive.
- Ukipenda tia mraba wa supu ya nyama - kidonge 1 (au supu yenyewe kiasi kidogo tu cha kutia ladha lakini hakikisha supu isizidishe kipimo kwa kupunguza maji au maziwa).
- Zima moto, tia nyanya na pilipili mboga.
- Bashamela
- Katika sufuria tia siagi weka katika moto.
- Tia unga na kaanga ugeuke rangi uwe rangi brauni khafifu.
- Tia maziwa na haraka haraka ukoroge kwa mchapo wa mayai kutoa madonge.
- Tia cheese. Ikiwa madonge hayakutoka tia katika mashine ya kusagia (blender) na usage kisha rudisha kidogo katika moto mdogo mdogo na huku unakoroga kwa mchapo wa mayai.
Kutayarisha Kuyapika
- Tia nusu ya sosi ya nyama chini ya bakuli la kupikia katika oveni.
- Tia nusu makaroni na mwagia nusu ya bashamela.
- Tia tena nusu nyingine ya nyama kisha tena makaroni kisha tena bashamela.
- Pika (bake) katika moto wa 400 Deg kwa muda wa dakika 15-20 hadi bashamela igeuke rangi kidogo.
- Epua ikiwa tayari kuliwa.