Chow Mein (Tambi Nene Za Kukaanga) Za Nyama Kusaga Na Mboga Mchanganyiko
Chow Mein (Tambi Nene Za Kukaanga) Za Nyama Kusaga Na Mboga Mchanganyiko
Vipimo
Noodles (Tambi nene za tayari) - 1 paketi (500 gm)
Nyama ya kusaga - 1 Lb
Mafuta ya ufuta (Sesame oil) - 3 vijiko vya supu
Njegere changa (Spring onions) - ½ kikombe
Karoti ilokatwakatwa - ½ kikombe
Mahindi - ½ kikombe
Maharage mabichi ya kijani - ½ kikombe
Sosi ya soya (soy sauce) - 3 vijiko vya supu
Sosi ya nyanya/Tomato ketchup - 3 vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) ilokunwa (grated) - 5 - 7 chembe
Tangawizi mbichi ilokunwa (grated) - 1 kipande
Pilipili manga - ½ kijiko cha chai
Paprika au pilipili nyekundu - ½ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Maji - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Chambua noodles (tambi nene). Ikiwa ni zilozongoreka zikatekate kama kwenye picha.
2. Chemsha maji na zipike kama inavyoelezwa katika paketi. Au chemsha kiasi ya dakika chache tu zisiive sana hadi zikawa laini sana. Chuja maji. Changanya na siagi ili zisigandane.
3. Weka mafuta katika kisufuria kisha tia kitunguu thomu na tangawizi , kaanga harakaharaka kidogo tu kisha tia sosi zote, endelea kukaanga kidogo tu.
4. Tia nyama ya kusaga kaanga.
5. Tia mboga zote, na maji kisha funika mboga ziive.
6. Katika bakuli kubwa mimini tambi kisha changanya pamoja na sosi ya nyama ya kusaga ikiwa tayari.
Kidokezo:
Sio lazima kupatikana tambi za aina hiyo ya paketi. Muhimu ni tambi zozote nene (noodles)