Sphagetti Kwa Sosi Ya Fasulia (Maharage Machanga) Na Kabaab Za Kukaanga
Sphagetti Kwa Sosi Ya Fasulia Na Kabaab Za Kukaanga
Vipimo
Sphagetti - 1 paketi
Vipimo vya Kababu
Nyama ya kusaga - ½ kilo
Tangawizi mbichi ilosagwa - 2 vijiko vya kulia
Bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha kulia
Pilipili mbichi ya kijani ilosagwa - 2-3
Chumvi - kiasi
Kotmiri katakata - kiasi
Mayai - 2
Slesi ya mkate - 4-5
Mafuta ya kukaangia
Vipimo Vya Sosi
Fasulia (maharage meupe machanga) - 1 kikombe
Kitunguu kilokatwakatwa - 2
Nyanya zilokatwakatwa - 3
Nyanya ya paste – tomatoe paste - 3 vijiko vya kulia
Pilipili boga la kijani - 1
Herbs: Nanaa kavu, organo, zaatari - ½ kijiko cha chai kila moja
Mafuta - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Kabaab:
- Roweka slesi za mkate katika bakuli dogo, kamua maji na chuja.
- Katika bakuli changanya vitu vya kabaab pamoja na mkate ulokamua.
- Fanya duara anza kukaanga moja kwanza, ukiona haishiki, ongezea unga wa dengu kijiko kimoja cha kulia.
- Kaanga katika mafuta kwenye karai.
Sosi Ya Fasulia
- Roweka fasulia (maharage machanga) kisha chemsha yawive.
- Weka mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu mpaka vianze kugeuka rangi.
- Tia nyanya kaanga ziive kisha tia nyanya paste na vitu vingineyo kaanga kidogo.
- Changanya na fasulia sosi ikiwa tayari.
- Chemsha sphagetti, tia mafuta kidogo unapochemsha.
- Mwaga maji uchuje kisha pakua katika chombo.
- Pakua kwenye sahani sphagetti, mwagia sosi ya fasulia na weka kabaab juu yake.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)