Spageti Na Sosi Ya Nyama Ng'ombe Vipande
Spageti Na Sosi Ya Nyama Ng'ombe Vipande
Vipimo
Spaghetti - 500g
Maji - 1lita na nusu
Chumvi - 1 kijiko cha supu
Tomato ya kopo - 3 Vijiko vya supu
Tomato (fresh) - 3
Kitunguu maji - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Nyama bila mifupa - nusu kilo
Tangawizi mbichi ilyosagwa - 1 kijiko cha supu
Mafuta - nusu kikombe cha chai
Namna ya kutayarisha sosi
- Nyama ikoshe na ukata vipande (size) upendayo,tia sufuriani.
- Itie tangawizi,chumvi nusu, na ipike kwa kuikausha moto wa chini bila kuongeza chochote paka itoe maji na kutowa harufu ya supu zima jiko.
- Kwenye sufuria nyengine katakata tomato, kitunguu,tia mafuta nusu mengine utatia kwenye spaghetti.
- Weka jikoni ongeza thomu,tomato ya kopo kijiko kimoja na pika kwa nusu saa.
- Saga mchanganyo wa mboga ulopika kwa machine ya kusagia (handy mixer); paka isagike kisha ongeza tena tomato ya kopo ilobakia usisage tena hapa.
- Rojo lile la mboga, mimina nyama changanya na rudisha kwenye jiko kwa moto wa chini na iache ipikike kwa muda wa dakika 45 – 50; Na sosi itakuwa tayari.
Spaghetti
- Sufuria ya nafasi tia maji weka katika jiko yaache mpaka yachemke kisha mimina spaghetti.Ziache mpaka ziive toa moja ubonyeze ukiona imewiva ,chuja maji yote.
- Rudisha sufuriani kisha mimina chumvi na mafuta ulobakisha zipepete zichanganyike mafuta vizuri.Tayari kuliwa.
Kidokezo
Unaweza kukwaruza cheese kwenye spaghetti baada ya kupakuwa kama kwenye picha.