Makaroni Ya Nyama Ya Kusaga Kwa Jibini Na Sosi Ya Bashamel
Makaroni Ya Nyama Ya Kusaga Kwa Jibini Na Sosi Ya Bashamel
Vipimo
Makaroni (aina yoyote) - 1 Pakti (950) gms
Vipimo Vya Sosi
Nyama ya kusaga - 1 Kilo
kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi iliyosagwa - 2 vijiko vya chai
Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai
Vitumguu maji - 2
chumvi - kiasi
Mafuta ya kupikia - 1/4 kikombe
Sosi ya macaroni - 1 kopo (680) gm
Mraba ya supu ya nyama - kidonge 1 (au supu yenyewe kiasi kidogo tu cha kutia ladha lakini hakikisha supu isizidishe kipimo).
Garam masala - 1 Kijiko cha chai
Dania ya unga - 1 Kijiko cha chai
Kotmiri - 2 Vijiko vya Supu
Pilipili ya unga - 1 Kijiko cha chai
Ndimu - 2 Vijiko vya supu
Ikibidi: unaweza kutumia nyanya ya kopo badala ya sosi ya makaroni
Namna Yakutayarisha
- Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitungu, tia thomu na tangawizi kisha tia nyama ya kusaga vilevile mbichi wacha ikaangike kisha tia bizari zote isipokuwa sosi ya makaroni.
- Halafu tia sosi ya makaroni wacha ichemke mpaka sosi iwe mzito.
Vipimo Vya Bashamel
Unga mweupe - 4 Vijiko vya supu
Siagi (butter) - 3 vijiko vya supu
Maziwa - 1 lita
Pilipili manga - ½ kijiko cha chai
Mayonezi - 2 Vijiko vya supu
Jibini iliyokunwa(Grated Cheese) - 2 Vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha
- Tia unga katika sufuria siagi na mafuta kaanga kidogo .
- Tia maziwa koroga kwa mwiko na usage ili uondoshe madonge mpaka uwe mzito kama uji.
- Kisha tia mayonezi , pilipili manga na jibini ilikwanguliwa.
- * Iwe kazi ya mwisho kutayarisha sosi, umwagie katika makoroni ukiwa tayari umeshapanga kila kitu.
Vya Kumwagia Ndani Na Juu Ya Makaroni
Jibini zote ziwe zimekunwa (grated)
Jibini ya cheddar (cheddar cheese) - 200 – 250 gm
Jibini ya mazorella (mozorella cheese) - 200 –250 gm
Utakuwa Umetayarisha Vitu Hivi Viwe Tayari
- Sosi ya nyama ya kusaga
- Makaroni yaliyochemshwa yakaiva
- Sosi ya Bashamel
- Jibini iliyokunwa (shredded cheese)
- Mapilipili mboga ya rangi tofauti.
Kumalizia Kupika Makaroni
- Panga nusu makaroni katika bakuli au trea ya kupikia katika oveni.
- Tia nusu ya sosi ya nyama
- Tia nusu ya jibini iliyokunwa
- Tia tena makaroni yaliyobaki
- Malizia kwa kumwagia sosi ya bashamel hakikisha inaingia pande zote na ndani ya makaroni.
- Pambia kwa Mapilipili mboga yaliyokatwakatwa.
- Malizia juu yake jibini iliyobaki
- Tia kwenye oven kwa moto wa 350 ˚C kwa muda wa dakika 15 mpaka 20 mpaka jibini iyayuke
- Epua ikiwa tayari kuliwa.
Kidokezo:
Unaweza kutumia sosi ya pasta ya tayari ila uongeze nyama ya kusaga uliyoikausha kwa viungo.