Macaroni Ya Express Ya Kidari Cha Kuku
Macaroni Ya Express Ya Kidari Cha Kuku Na Jibini
Vipimo
Makaroni - 500 gm
Kidari cha kuku katakata vipande - ½ kilo
Kitunguu katakata kidogodogo - 1
Nyanya/tungule katakata ndogo ndogo - 3
Thomu (garlic) ilosagwa - 1 kijiko cha chai
Nyanya kopo (paste) - 1 kijiko cha kulia
Pilipili nyekundu ya unga - ½ kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia - 3 vijiko cha kulia
Jibini (Cheese) iliyokunwa ya cheddar - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Weka mafuta katika sufuria yakishika moto kaanga vitunguu mpaka vilainike.
-
Tia thomu (kitunguu saumu) endelea kukaanga kwa dakika moja.
-
Tia kuku, chumvi, pilipili na endelea kukaanga au kukoroga. Acha ipikike bila kuifunika mpaka kuku aive.
-
Tia nyanya, changanya ukoroge mpaka nyanya ziive na kuwa laini kisha tia nyanya kopo.
-
Tia macaroni, koroga, kisha tia maji kiasi yafunike macaroni. Koroga kisha funika na punguza moto uwe mdogo.
-
Pika kwa dakika 15, koroga kisha tazama kama macaroni yameiva na maji yamekauka. Yakiwa hayakuiva bado ongezea maji lakini yasizidi ¼ kikombe. Na yakiwa yameiva na bado yana maji, funua mfuniko upike wazi ili maji yakauke.
-
Zima moto, kisha changanya na jibini (cheese) kisha pakua katika chombo yakiwa tayari.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)