Lasagna
Lasagna
Vipimo
*Pasta ya Lasagna ya tayari - 1 paketi 500 – 600 gms
Nyama ya kusaga - 1 Lb (1/2 kilo)
Kitunguu kilichokatwakatwa (chopped) - 1
Nyanya zilizokatwakatwa (chopped) - 3
Nyanya kopo (paste) - 2 vijiko vya chai
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
*Nanaa iliyokatwakatwa (chopped) - 1 msongo (bunch)
*Oregano - ½ kijiko cha chai
*Zaatari (thyme) - 1 kijiko cha chai
*Basil (majani ya mrehani) - ½ kijiko
* Parsley - 1 msongo (bunch)
Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga - 1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Mafuta ya zaytuni (olive oil) - ¼ kikombe
Jibini ya mazorella iliyochunwa (grated) - 500 gms
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Weka mafuta katika kisufuria, kisha kakaanga kitunguu hadi kigeuke rangi kidogo.
- Tia thomu endelea kukaanga, kisha tia nyama, pilipili manga, mdalasini, chumvi na endelea tena kukaanga hadi karibu na kuwiva.
- Tia nyanya, nyanya kopo na viungo vyote vilobakia, endelea kukaanga kidogo kisha epua sufuria weka kando, sosi ikiwa tayari.
- Chemsha lasagna katika maji ya moto kama ilivyo maelezo katika paketi. Chuja kwa kumwaga maji.
- Panga miraba ya lasagna na sosi katika treya ya kupikia ndani ya oven (oven proof). Weka kwanza miraba ya lasagna kiasi ifunike sehemu ya chini ya treya.
- Tia nusu ya sosi utandaze vizuri kote.
- Mwagia jibini kiasi utandaze vizuri.
- Panga tena juu yake miraba ya lasagna, urudie tena kama mwanzo kuweka sosi iliyobakia, kisha jibini.
- Mwisho weka tena miraba ya lasagna na jibini pekee kisha ipike lasagna katika oveni (Bake) kwa moto wa kiasi cha 350-400° C kwa muda wa nusu saa. Epua ikiwa tayari.
Kidokezo:
* Unaweza kutumia viungo vya tayari vya Kiitali