Makaroni Ya Zuchini Na Sosi Ya Nyama Ng’ombe
Makaroni Ya Zuchini Na Sosi Ya Nyama Ng’ombe
Makaroni
Vipimo na Namna ya Kuatayarisha
Makaroni - 500 gms
Kitunguu maji Katakata (chop) - 1
Nyanya/tungule Katakata vipande vidogodogo (dice) - 3
Kitunguu saumu (thomu) Saga au katakata (chop) - 1 kijiko cha supu
Zuchini - kata slesi za round - 2
Pilipili boga (capsicum) katakakata - 1
Chumvi Kisia
Pilipili manga - 1 kijiko cha chai
Mafuta - 2 vijiko vya supu
Namna Ya Kupika:
- Chemsha makaroni yaive, chuja maji. Tia siagi kidogo yasigandane.
- Katika sufuria, weka mafuta, kaanga vitunguu hadi vilainike na kugeuka rangi kidogo.
- Tia kitunguu thomu kaanga.
- Tia nyanya, pilipili manga, chumvi changanya vizuri.
- Tia slesi za zuchini, na pilipili boga funika kidogo viive kidogo.
- Tia makaroni, changanya vizuri yakiwa tayari kuliwa na sosi ya nyama.
Sosi Ya Nyama:
Vipimo na Namna ya Kutayarisha
Nyama ng’ombe Katakata vipande vidogo kiasi - ½ kilo
Tangawizi mbichi saga - 1 kijiko cha chai
Kitunguu saumu (thomu) saga - 1 kijiko cha chai
Kitunguu Katakata (chop) - 1
Nyanya kopo (paste) - 3 vijiko vya supu
Kotmiri - Katakata (chop) - ½ kikombe cha chai
Oregano (bizari ya pasta) - 1 kijiko cha chai
Namna Ya Kupika
- Weka nyama katika sufuria, tia tangawizi mbichi, kitunguu thomu, chumvi changanya vizuri.
- Funika uchemshe nyama hadi iwive na kukaribia kukauka.
- Tia mafuta, vitunguu, nyanya, nyanya kopo, oregano, changanya vizuri uendelee kupika.
- Ikiwiva tia kotmiri, zima moto ikiwa tayari kuliwa na makaroni.