Chow Mein Za Kuku Pilipili Boga Mahindi (Guyana)
Chow Mein Za Kuku Pilipili Boga Mahindi (Guyana)
Vipimo na namna ya kutayarisha
Tambi nene Chambua katakata - 500 gms
Kuku bila mifupa (kidari) Katakata vipande vipande - 1 Lb/ ½ Kilo
Mahindi Chambua - 1 kikombe
Pilipili boga jekundu (capsicum)Katakata - 1
Pilipili boga la orengi Katakata – 1
Tangawizi mbichi kuna (grate) - 1 kijiko cha supu
Kitunguu saumu (thomu) kuna (grate) - 1 kijiko cha supu
Pilipil manga ya unga - 1 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga - ½ kijiko cha chai
Bizari manjano/haldi/tumeric - 1 kijiko cha chai
Sosi ya soya (soy sauce) - 2 vijiko vya supu
Chumvi - Kisia
Mafuta - ¼ kikombe
Namna Ya Kupika:
- Chemsha tambi, ziwive kiasi, mwaga maji, chuja. Tia siagi ili zisigandane.
- Chemsha chembe za mahindi kidogo tu kiasi ya kuivisha. Mwaga maji chuja.
- Weka mafuta katika karai, pasha moto, kisha tia tangawizi mbichi na kitunguu thomu kaanga kidogo tu, kisha haraka tia kuku, sosi ya soya, bizari, pilipili manga, chumvi.
- Funika kuku awive huku unafungua kumkaanga.
- Karibu na kuwiva tia pilipili boga na mahindi.
- Tia tambi changanya vizuri kisha pakua katika chombo.
Picha za aina ya tambi zinapatikana katika viungo vifuatavyo:
Chow Mein (Tambi Nene Za Kukaanga) Za Nyama Kusaga Na Mboga Mchanganyiko
Chow Mein (Tambi Nene Za Kukaanga) Za Kamba Na Mboga Mchanganyiko