Moussaka Bilingani Kwa Sosi Ya Nyanya Beshamel Na Jibini
Moussaka Bilingani Kwa Sosi Ya Nyanya Beshamel Na Jibini
Vipimo
Nyama ya kusaga - ¼ kilo
Bilingani - 4 kubwa
Kitunguu kilokatwakatwa - 2
Nyanya – katakakata - 4
Pilipili boga (capsicum) - 1
Tangawizi mbichi ilokunwa au kusagwa - 1 kipande
Nyanya kopo - 1 kijiko cha supu
Herbs ya oregano - 1 kijiko cha chai
Nanaa kavu (dry mint) - ½ kijiko cha chai
Pilipili manga - 1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Jibini ya cheddar au mazorella - 500 gms
Mafuta - 3 vijiko vya kulia
Mafuta ya kukaangia bilingani - Kiasi
Sosi ya beshamel:
Unga - vijiko 3 vya kulia
Siagi - vijiko 2 vya kulia
Maziwa - kiasi gilasi 3
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha nyama kiasi uichuje
- Kata bilingani slices ndefu. Kaanga katika mafuta mengi yaliyo yamoto, Epua uchuje mafuta.
- Weka mafuta vijiko 3 katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kidogo.
- Tia nyama, na tangawizi uchanganye vizuri, kakaanga kidogo.
- Tia nyanya na viungo vyote isipokuwa jibini. Kaanga kidogo. Epua
- Panga nusu ya slesi za bilingani katika bakuli la kupikia ndani ya oven.
7. Mwagia sosi juu yake kisha kuna jibini (cheese) umwagie juu yake.
8. Panga tena slesi za bilingani kisha mwagia sosi ya beshamel kisha jibini tena.
9. Weka ndani ya oven upike (bake) kwa moto mdogo wa kiasi mpaka igeuke rangi kidogo.
10. Epua ipoe, ikiwa tayari.
Namna ya kutengeneza sosi ya beshamel
- Weka siagi katika sufuria, tia unga weka katika moto, kaanga ugeuke rangi.Tia maziwa
- na kidonge cha supu ukoroge usiachie mkono mpaka uive.
- Epua utumie kumwagia katika moussaka au pasta yoyote ile.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)