Makaroni Ya Kuku Na Bashamel (Sosi Nyeupe)
Makaroni Ya Kuku Na Bashamel (Sosi Nyeupe)
Vipimo
Makaroni (aina yoyote) - 500 gms
Kuku:
Nyama ya kuku bila mafupa
iliyokatwa ndogo ndogo -1LB
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai
chumvi - kiasi
Vipimo vya Sosi
Mafuta ya kupikia - 1/4 kikombe
Nyanya – kata ndogo ndogo - 4
Nyanya kopo - 4 vijiko vya supu
Kechapu ya nyanya (tomato ketchup) - 5 vijiko vya supu
Supu ya kuku ya vidonge:
Mraba ya supu ya kuku au nyama - kidonge 1, au supu yenyewe kiasi cha kutia ladha (hakikisha supu isizidi kipimo).
Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai
Viungo vya Kiitali ukipenda
(Italian spices; Oregano, mint, thyme) - 1 kijiko cha supu
Namna ya kutayarisha
- Mtie kuku chumvi, pilipili manga, thomu, mpike awive. (Unaweza kutumia kidari au sehemu yoyote ya kuku, ukishaipika utoe mafupa na uchambue nyama ndogo ndogo)
- Epua weka kando.
- Tia mafuta katika sufuria, kaanga nyanya, tia nyanya kopo, kechapu, viungo vya kiitali, pilipilimanga , chumvi na kidonge cha supu (Maggi cube).
- Pika hadi sosi iwe tayari isiwe nzito sana, ongeza maji 1/2 kikombe.
*Vipimo vya Bashamel
Unga mweupe - 1/2 kikombe
Siagi (butter) - 3 vijiko vya supu
Maziwa - 2 vikombe vikubwa (mugs)
Kidonge cha supu (Maggi cube) - 1
Namna ya kutayarisha
- Tia unga katika sufuria.
- Tia siagi kaanga kidogo ubadilike rangi unga uwe rangi ya hudhurungi hafifu. (light brown)
- Tia maziwa koroga kwa mwiko wa kupigia mayai au tia katika mashine ya kusagia (blender) na usage ili uondoshe madonge.
- Tia kidonge cha supu (Maggi cube) kisha rudisha katika moto kidogo uipike sosi. Isiwe nzito sana iwe kama kastadi na kama nzito sana ongeza maziwa.
- * Iwe kazi ya mwisho kutayarisha sosi, umwagie katika makoroni ukiwa tayari umeshapanga kila kitu.
Vya kumwagia ndani na juu ya makaroni
Jibini zote ziwe zimekunwa (grated)
Jibini ya cheddar (cheddar cheese) - 200 – 250 gm
Jibini ya mazorella (mozorella cheese) - 200 –250 gm
Utakuwa umetayarisha vitu hivi viwe tayari
Kuku aliyepikwa na kuchambuliwa
Sosi ya nyanya
Makaroni yaliyochemshwa yakaiva
Sosi ya Bashamel
Jibini iliyokunwa (shredded cheese)
Kumalizia kupika makaroni
- Panga nusu makaroni katika bakuli au trea ya kupikia katika oveni.
- Tia nusu ya sosi ya nyanya
- Tia nusu ya kuku aliyechambuliwa
- Tia nusu ya jibini iliyokunwa
- Rudia kupanga tena kwa mpangilio huo huo.
- Malizia kwa kumwagia sosi ya bashamel hakikisha inaingia pande zote na ndani ya makaroni.
- Pambia kwa viungo vya kiitali au naanaa (mint) iliyokatwa ndogo ndogo.
- Pika katika oveni moto wa 350-400º kwa muda wa dakika 15-20 hadi jibini sosi ya bashamel iwive.
- Epua ikiwa tayari kuliwa.