42-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Anapotokwa Na Majimaji Je Inatosha Aoshe Viungo Vya Wudhuu Pekee?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
42-Anapotokwa Na Majimaji Je Inatosha Aoshe Viungo Vya Wudhuu Pekee?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Kuhusuana na udhu wa majimaji hayo je itatosheleza kukosha viungo vya udhu tu?
JIBU:
Naam, itatosheleza hilo pindi ikiwa ni tohara nayo ni ambayo inatoka kwenye nyumba ya kizazi na sio kwenye kinena.
