028-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kusitiri Aibu Za Waislamu Na Katazo La Kuzieneza Pasi Na Dharura

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب ستر عورات المسلمين والنهي عن إشاعتها لغير ضرورة

028-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kusitiri Aibu Za Waislamu Na Katazo La Kuzieneza Pasi Na Dharura

 

Alhidaaya.com

 

 

قَالَ الله تَعَالَى :

إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿١٩﴾

Hakika wale wanaopenda uenee uchafu wa kashfa kwa wale walioamini; watapata adhabu iumizayo duniani na Aakhirah. Na Allaah Anajua nanyi hamjui. [An-Nuur: 19]

 

 

Hadiyth – 1

وعن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال‏: ((لاَ يَسْتُرُ عَبْدٌ عَبْداً في الدُّنْيَا إلاَّ سَتَرَهُ اللهُ يَوْمَ القِيَامَةِ)) ‏‏  ‏رواه مسلم‏.‏‏

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah  (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mja hatamstiri mja mwenziwe duniani ila Allaah Atamstiri yeye Siku ya Qiyaamah." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أبي هريرة رضي الله عنه قال‏:‏ سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول‏:‏ ‏ ((‏كُلُّ أُمَّتِي مُعَافى :إلاَّ المُجَاهِرِينَ ، وَإنّ مِنَ المُجَاهَرَةِ أنْ يَعْمَلَ الرَّجُلُ باللَّيلِ عَمَلاً ، ثُمَّ يُصْبحُ وَقَدْ سَتَرَهُ اللهُ عَلَيهِ ، فَيقُولُ يَا فُلانُ ، عَمِلت البَارِحَةَ كَذَا وَكَذَا ، وَقَدْ بَاتَ يَسْتُرُهُ رَبُّهُ ، وَيُصبحُ يَكْشِفُ ستْرَ اللهِ عَنْه‏)).‏ ‏متفق عليه‏ ‏.

Na kutoka  kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) alisema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Ummah wangu wote umesalimika ila wanaodhihirisha (maovu) ni mtu kutenda amali (ya maasiya) usiku kisha apambazukiwa ilhali amesitiriwa na Allaah, asema: 'Ee fulani, usiku wa jana nilifanya kadha na kadha.' Na hakika alikuwa amepitiwa na usiku mzima akiwa amesitiriwa na Rabb wake, na anapambazukiwa akiifunua sitara aliyositiriwa na Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ‏((إِذَا زَنَتِ الأَمَةُ فَتَبيَّنَ زِنَاهَا فَلْيَجْلِدْهَا الحَدَّ ، وَلا يُثَرِّبْ عَلَيْهَا ، ثُمَّ إنْ زَنَتِ الثَّانِيَةَ فَلْيَجْلِدْهَا الحَدَّ ، وَلا يُثَرِّبْ عَلَيْهَا ، ثُمَّ إنْ زَنَتِ الثَّالِثَةَ فَلْيَبِعْهَا وَلَوْ بِحَبْل مِنْ شَعَر‏)).‏ ‏‏متفق عليه‏ ‏.‏ 

Na kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Pindi atakapozini kijakazi na ikabainika zinaa yake, basi apigwe mijeledi ya adhabu (iliyowekwa na Shariy’ah) wala asikaripiwe. Kisha akizini mara ya pili apigwe tena mijeledi ya adhabu wala asikaripiwe. Kisha akizini tena mara ya tatu, amuuze kwa japokuwa kwa kamba iliyotengenezwa kwa nywele." [Al Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: أُتِيَ النَّبيّ  صلى الله عليه وسلم برجل قَدْ شَرِبَ خَمْراً ، قَالَ ‏:‏‏((اضْربُوهُ)) قَالَ أَبُو هريرة : فَمِنَّا الضَّارِبُ بِيَدِهِ ، والضَّارِبُ بِنَعْلِهِ ، وَالضَّارِبُ بِثَوبِهِ . فَلَمَّا انْصَرَفَ ، قَالَ بَعضُ القَومِ : أخْزَاكَ الله ، قَالَ  (( لا تَقُولُوا هكَذا ، لاَ تُعِينُوا عَلَيهِ الشَّيْطَانَ‏)).‏ ‏‏رواه البخاري‏‏‏.

Na kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiyah Allaah 'anhu) amesema: Aliletwa mtu mlevi kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akasema: "Mpigeni." Akasema Abuu Hurayrah: Wapo miongoni mwetu waliompiga kwa mkono wake, wengine kwa viatu vyao na wengine kwa nguo zao. Alipoondoka (huyu mtu) walisema baadhi ya watu: "Allaah akupe hizaya (akudhililishe). "Akasema "Msiseme hivyo, msimsaidie shetani dhidi yake." [Al Bukhaariy]

 

 

 

Share