029-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuwakidhia Waislamu Haja Zao
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب قضاء حوائج المسلمين
029-Mlango Wa Kuwakidhia Waislamu Haja Zao
قَالَ الله تَعَالَى
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا وَاعْبُدُوا رَبَّكُمْ وَافْعَلُوا الْخَيْرَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ۩﴿٧٧﴾
Enyi walioamini! Rukuuni, na sujuduni na mwabuduni Rabb wenu, na fanyeni ya khayr ili mpata kufaulu. [Al-Hajj: 77]
Hadiyth – 1
وعن ابن عمر رضي الله عنهما أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((المُسْلِمُ أخُو المُسْلِمِ ، لاَ يَظْلِمُهُ وَلاَ يُسْلِمُهُ . مَنْ كَانَ في حَاجَة أخِيه ، كَانَ اللهُ في حَاجَتِهِ، وَمَنْ فَرَّجَ عَنْ مُسْلِمٍ كُرْبَةً، فَرَّجَ اللهُ عَنْهُ بِهَا كُرْبَةً مِنْ كرَبِ يَومِ القِيَامَةِ ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِماً سَتَرَهُ اللهُ يَومَ القِيَامَةِ )). متفق عليه .
Na imepokewa kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Muislamu ni ndugu yake Muislamu, hamdhulumu wala hamsalimishi (kwa adui). Mwenye kumtekelezea haja nduguye Allaah Atamtekelezea haja yake. Na mwenye kumwondolea Muislamu dhiki, Allaah Atamwondolea dhiki miongoni mwa dhiki za Siku ya Qiyaamah. Na mwenye kumsitiri Muislamu, Allaah Atamsitiri Siku ya Qiyaamah." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: (( مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤْمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنيَا ، نَفَّسَ الله عَنْهُ كُربَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ القِيَامَةِ ، وَمَنْ يَسَّر عَلَى مُعْسِرٍ يَسَّرَ الله عَلَيهِ في الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِماً سَتَرَهُ الله في الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ ، والله في عَونِ العَبْدِ مَا كَانَ العَبْدُ في عَونِ أخِيهِ ، وَمَنْ سَلَكَ طَريقاً يَلْتَمِسُ فِيهِ عِلْماً سَهَّلَ اللهُ لَهُ طَريقاً إِلَى الجَنَّةِ . وَمَا اجْتَمَعَ قَوْمٌ في بَيت مِنْ بُيُوتِ اللهِ تَعَالَى ، يَتْلُونَ كِتَابَ اللهِ ، وَيَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ إلاَّ نَزَلَتْ عَلَيْهِمُ السَّكِينَةُ ، وَغَشِيتْهُمُ الرَّحْمَةُ ، وَحَفَّتْهُمُ المَلاَئِكَةُ ، وَذَكَرَهُمُ الله فِيمَنْ عِندَهُ . وَمَنْ بَطَّأ بِهِ عَمَلُهُ لَمْ يُسْرِع بِهِ نَسَبُهُ)) رواه مسلم
Imepokewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye kumfariji Muumini dhiki miongoni mwa dhiki za duniani, Allaah Atamfariji (na kumuondolea) dhiki miongoni mwa dhiki za Siku ya Qiyaamah. Na mwenye kumsahilishia mwenye uzito, Allaah Atamsahilishia duniani na Aakhirah. Na mwenye kumsitiri Muislamu, Allaah Atamsitiri duniani na Aakhirah. Na Allaah Anamsaidia mja huyu yu katika kumsaidia nduguye. Na mwenye kufuata njia akitafuta elimu katika njia hiyo, Allaah Atamsahilishia njia ya kwenda Jannah. Na watu hawatakusanyika katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah (Ta’aalaa) wakisoma kitabu cha Allaah na wakifundishana isipokuwa huteremka utulivu, wakafunikwa na Malaika na Allaah Akawataja kwa walio Kwake. Na anayechelewesha na amali yake hatopelekwa mbele kwa nasaba yake.” [Muslim na Ahmad].