038-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Wajibu Wa Kuamrisha Mkewe, Wanawe Waliobaleghe na Wote Waliochini Yake Kumtii Allaah Aliyetukuka, na Kuwakataza Kukhalifu, na Kufanya Waliyokatazwa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب وجوب أمره أهله وأولاده المميزين

وسائر من في رعيته بطاعة الله تعالى ونهيهم عن المخالفة وتأديبهم

ومنعهم من ارتكاب مَنْهِيٍّ عَنْهُ

038-Mlango Wa Wajibu Wa Kuamrisha Mkewe, Wanawe Waliobaleghe na Wote Waliochini Yake Kumtii Allaah Aliyetukuka, na Kuwakataza Kukhalifu, na Kufanya Waliyokatazwa

 

Alhidaaya.com

 

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَأْمُرْ أَهْلَكَ بِالصَّلَاةِ وَاصْطَبِرْ عَلَيْهَا ﴿١٣٢﴾

Na amrisha ahli zako Swalaah, na dumisha kusubiri kwayo. Hatukuombi riziki. Sisi Ndio Tunaokuruzuku. Na khatima njema ni kwa wenye taqwa. [Twaahaa: 132]

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا ﴿٦﴾

Enyi walioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na moto. [At-Tahriym: 6]

 

 

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : أخذ الحسن بن علي رضي الله عنهما تَمْرَةً مِنْ تَمْر الصَّدَقَةِ فَجَعَلَهَا في فِيهِ ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( كَخْ كَخْ إرْمِ بِهَا ، أمَا عَلِمْتَ أنَّا لا نَأكُلُ الصَّدَقَةَ !؟ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : (( أنَّا لا تَحِلُّ لَنَا الصَّدَقَةُ )) .

Amesema Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Al-Hasan bin 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) Alichukua tende ya sadaqah akaitia mdomoni mwake akitaka kuila. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akamwambia: "Kikh! Kikh! Itupe, kwani hujui kuwa sisi hatuli sadaqah? [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

Katika riwaayah nyingine: "Sadaqah si halali kwetu sisi."

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي حفص عمر بن أَبي سلمة عبد الله بن عبد الأسدِ ربيبِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : كُنْتُ غلاَماً في حجر رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وَكَانَتْ يَدي تَطِيشُ في الصَّحْفَةِ ، فَقَالَ لي رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( يَا غُلامُ ، سَمِّ الله تَعَالَى ، وَكُلْ بيَمِينكَ ، وَكُلْ مِمَّا يَلِيكَ )) فَمَا زَالَتْ تِلْكَ طِعْمَتي بَعْدُ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Abu afswi 'Umar bin Abu Salamah 'Abdillaah bin 'Abdil Asad (Radhwiya Allaahu 'anhu) mwanakambo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nilikuwa mvulana katika nyumba ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), mkono wangu ulikuwa unazunguka kwenye sinia. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akaniambia: "Ee kijana! Mtaje Allaah Aliyetukuka, na kula kwa kulia kwako, na kula cha mbele yako." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

Hadiyth – 3

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم،    يقول : (( كُلُّكُمْ رَاعٍ ، وَكُلُّكُمْ مسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتهِ : الإمَامُ رَاعٍ وَمَسْؤولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ ، والرَّجُلُ رَاعٍ في أهْلِهِ وَمَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ ، وَالمَرْأةُ رَاعِيَةٌ في بيْتِ زَوْجِهَا وَمَسْؤُولَةٌ عَنْ رَعِيَّتِهَا ، وَالخَادِمُ رَاعٍ في مَالِ سَيِّدِهِ وَمَسؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ ، فَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَمَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhummaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kila mmoja wenu ni mchunga, na kila mmoja wenu ataulizwa aliowachunga. Kiongozi ni mchunga ataulizwa aliowachunga, na mume ni mchunga kwa watu wa nyumbani kwake, na mke naye ni mchunga katika nyumba ya mumewe na watoto wake; hivyo kila mmoja wenu ni mchunga na nyote mtaulizwa kwa mlivyovichunga." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

Hadiyth – 4

وعن عمرو بن شعيب ، عن أبيه ، عن جدهِ رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مُرُوا أوْلادَكُمْ بِالصَّلاةِ وَهُمْ أبْنَاءُ سَبْعِ سِنينَ ، وَاضْرِبُوهُمْ عَلَيْهَا ، وَهُمْ أبْنَاءُ عَشْرٍ ، وَفَرِّقُوا بَيْنَهُمْ في المضَاجِعِ )) حديث حسن رواه أَبُو داود بإسناد حسن .

Na imepokewa kutoka kwa 'Amr bin Shu'ayb (Radhwiya Allaahu 'anhu) kutoka kwa babake kutoka kwa babu yake kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na miaka saba, na wapigeni (kuacha kuswali) wakiwa na miaka kumi na muwatenganishe katika malazi." [Hadiyth Hasan iliyonukuliwa na Abu Daawuud kwa Isnadi iliyo Hasan]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي ثُرَيَّةَ سَبْرَةَ بن معبدٍ الجُهَنِيِّ رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( عَلِّمُوا الصَّبِيَّ الصَّلاةَ لِسَبْعِ سِنِينَ ، وَاضْرِبُوهُ عَلَيْهَا ابْنَ عَشْرِ سِنِينَ )) حديث حسن رواه أَبُو داود والترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .

ولفظ أَبي داود : (( مُرُوا الصَّبِيَّ بِالصَّلاةِ إِذَا بَلَغَ سَبْعَ سِنِينَ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Thurayyah Sabrah bin Ma'bad Al-Juhaniyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wafundisheni watoto Swalaah wakiwa na miaka saba, na wachapeni (wakiacha na kupuuza) wakiwa na miaka kumi." [Hadiyth Hasan iliyonukuliwa na Abu Daawuud na At-Tirmidhiy, naye akasema ni Hadiyth Hasan]

Na lafdhi Abu Daawuud: "Waamrisheni watoto Swalaah wakifika miaka saba."

 

 

 

Share