039-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Haki Ya Jirani na Kumtendea Wema
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب حق الجار والوصية بِهِ
039-Mlango Wa Haki Ya Jirani na Kumtendea Wema
قَالَ الله تَعَالَى:
وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۗ ﴿٣٦﴾
Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na jirani mwenye ujamaa na jirani asiye na ujamaa na rafiki wa karibu, na msafiri aliyeishiwa masurufu, na wale iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. [An-Nisaa: 36]
Hadiyth – 1
وعن ابن عمر وعائشة رضي الله عنهما ، قالا : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَا زَالَ جِبْريلُ يُوصِيني بِالجَارِ حَتَّى ظَنَنْتُ أنَّهُ سَيُورِّثُهُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .
Kutoka kwa ibn 'Umar na 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhummaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuwacha Jibriyl kuniusia kuhusu jirani mpaka nikadhania kuwa atamrithisha (mali)." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي ذر رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( يَا أَبَا ذَرٍّ ، إِذَا طَبَخْتَ مَرَقَةً ، فَأكثِرْ مَاءهَا ، وَتَعَاهَدْ جيرَانَكَ )) رواه مسلم .
وفي رواية لَهُ عن أَبي ذررضي الله عنه، قَالَ : إنّ خليلي صلى الله عليه وسلم أوْصَاني : (( إِذَا طَبَخْتَ مَرَقَاً فَأكْثِرْ مَاءها ، ثُمَّ انْظُرْ أهْلَ بَيْتٍ مِنْ جِيرَانِكَ ، فَأصِبْهُمْ مِنْهَا بِمعرُوفٍ )) .
Na imepokewa na Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee Abu Dharr! Unapopika supu, ongeza maji, kisha utizame kama jirani yako (anahitajia)." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika riwaayah ya Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Hakika rafiki yangu, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameniusia: "Unapotengeneza supu ongeza maji, kisha tizama kama baadhi ya jirani zako (wanahitajia), kisha wapelekee sehemu yake kwa wema."
Hadiyth – 3
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( واللهِ لاَ يُؤْمِنُ ، وَاللهِ لاَ يُؤْمِنُ ، وَاللهِ لاَ يُؤْمِنُ ! )) قِيلَ : مَنْ يَا رَسُول الله ؟ قَالَ : (( الَّذِي لاَ يَأمَنُ جَارُهُ بَوَائِقَهُ ! )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .
وفي رواية لمسلم : (( لا يَدْخُلُ الجَنَّةَ مَنْ لاَ يَأمَنُ جَارُهُ بَوَائِقَهُ )) .
Imepokewa kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wa-Allaahi haamini! Wa-Allaahi haamini!Akaulizwa: "Nani Ee Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Ambaye jirani yake hasalimiki na shari zake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika riwaayah ya Muslim: "Hataingia Peponi ambaye jirani yake hasalimiki na shari zake."
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( يَا نِسَاء المُسْلِمَاتِ ، لاَ تَحْقِرَنَّ جَارةٌ لِجَارَتِهَا وَلَوْ فِرْسِنَ شَاة )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .
Na imepokewa kutoka kwake Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Enyi wanawake wa Kiislamu! Jirani asimdharau jirani yake hata kama amepika kwato za mbuzi." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لاَ يَمْنَعْ جَارٌ جَارَهُ أنْ يَغْرِزَ خَشَبَةً في جِدَارِهِ )) ، ثُمَّ يقُولُ أَبُو هريرة : مَا لِي أرَاكُمْ عَنْهَا مُعْرِضينَ ! وَاللهِ لأرْمِيَنَّ بِهَا بَيْنَ أكْتَافِكُمْ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Na imepokewa kutoka kwake Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Jirani asimkataze jirani kukita mbao katika ukuta wake." Abuu Hurayrah alikuwa akisema: "Mbona nawaona mumeipa mgongo Sunnah hii! Wa-Allaahi nitawaambia (hata mkichukia)." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 6
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بالله وَاليَومِ الآخرِ ، فَلاَ يُؤْذِ جَارَهُ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ باللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ باللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيَقُلْ خَيْراً أَوْ لِيَسْكُتْ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .
Na imepokewa kutoka kwake Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho asimuudhi jirani yake. Na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho amkirimu mgeni wake. Na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho aseme maneno ya kheri (mazuri) au anyamaze." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 7
وعن أَبي شُرَيْح الخُزَاعيِّ رضي الله عنه: أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مَنْ كَانَ يُؤمِنُ بِاللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيُحْسِنْ إِلَى جَارِهِ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ باللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيَقُلْ خَيْراً أَوْ لِيَسْكُتْ )) رواه مسلم بهذا اللفظ ، وروى البخاري بعضه .
Imepokewa kutoka kwa Abu Shuraykh Al-Khuzaa'iyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuwa anamuamini Allaah na Siku ya Mwisho, amfanyie hisani jirani yake. Na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho amkirimu mgeni wake. Na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho asema maneno ya kheri (mazuri) au anyamaze." [Muslim kwa lafdhi hii, na Al-Bukhaariy baadhi yake]
Hadiyth – 8
وعن عائشة رضي الله عنها ، قَالَت : قُلْتُ : يَا رَسُول الله ، إنَّ لِي جارَيْنِ ، فإلى أيِّهِمَا أُهْدِي ؟ قَالَ : (( إِلَى أقْرَبِهِمَا مِنكِ بَاباً )) رواه البخاري .
Kutoka kwa 'Aa'ishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) Amesema: Nilisema: "Ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hakika mimi nina majirani wawili, ni yupi kati yao nimpelekee zawadi?" Akasema: "Ambaye mlango wake uko karibu zaidi nawe." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 9
وعن عبدِ الله بن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( خَيْرُ الأَصْحَابِ عِنْدَ الله تَعَالَى خَيْرُهُمْ لِصَاحِبِهِ ، وَخَيرُ الجِيرَانِ عِنْدَ الله تَعَالَى خَيْرُهُمْ لِجَارِهِ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwake 'Abdillaahi bin 'Amr bin Al-'Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mbora kabisa wa sahibu mbele ya Allaah Aliyetukuka ni aliye bora kwa sahibu yake. Na mbora mno wa jirani mbele ya Allaah Aliyetukuka ni aliye bora kwa jirani yake." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]