042-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuwafanyia Wema Marafiki wa Baba na Mama, Jamaa, Mkw na Wote Wanaopendekezwa Kuwafanyia Ukarimu

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل بر أصدقاء الأب والأم والأقارب والزوجة وسائر من يندب إكرامه

042-Mlango Wa Kuwafanyia Wema Marafiki wa Baba na Mama, Jamaa, Mkw na Wote Wanaopendekezwa Kuwafanyia Ukarimu

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Hadiyth – 1

عن ابن عمر رضي الله عنهما : أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إنّ أبَرَّ البرِّ أنْ يَصِلَ الرَّجُلُ وُدَّ أبيهِ )) .رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika wema mkubwa kabisa ni mtu kuwaunga vipenzi wa baba yake." [Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 2

وعن عبد الله بن دينار ، عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رَجُلاً مِنَ الأعْرَابِ لَقِيَهُ بطَريق مَكَّةَ ، فَسَلَّمَ عَلَيهِ عبدُ الله بْنُ عُمَرَ ، وَحَمَلَهُ عَلَى حِمَارٍ كَانَ يَرْكَبُهُ ، وَأعْطَاهُ عِمَامَةً كَانَتْ عَلَى رَأسِهِ ، قَالَ ابنُ دِينَار : فَقُلْنَا لَهُ : أصْلَحَكَ الله ، إنَّهُمُ الأعرَابُ وَهُمْ يَرْضَوْنَ باليَسير ، فَقَالَ عبد الله بن عمر : إن أَبَا هَذَا كَانَ وُدّاً لِعُمَرَ بنِ الخطاب رضي الله عنه، وإنِّي سَمِعتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( إنَّ أبرَّ البِرِّ صِلَةُ الرَّجُلِ أهْلَ وُدِّ أبِيهِ )) .

وفي رواية عن ابن دينار ، عن ابن عمر : أنَّهُ كَانَ إِذَا خَرَجَ إِلَى مَكّةَ كَانَ لَهُ حِمَارٌ يَتَرَوَّحُ عَلَيهِ إِذَا مَلَّ رُكُوبَ الرَّاحِلةِ ، وَعِمَامَةٌ يَشُدُّ بِهَا رَأسَهُ ، فَبيْنَا هُوَ يَوماً عَلَى ذلِكَ الحِمَارِ إِذْ مَرَّ بِهِ أعْرابيٌّ ، فَقَالَ : ألَسْتَ فُلاَنَ بْنَ فُلاَن ؟ قَالَ : بَلَى . فَأعْطَاهُ الحِمَارَ ، فَقَالَ : ارْكَبْ هَذَا ، وَأعْطَاهُ العِمَامَةَ وَقالَ : اشْدُدْ بِهَا رَأسَكَ ، فَقَالَ لَهُ بعضُ أصْحَابِهِ : غَفَرَ الله لَكَ أعْطَيْتَ هَذَا الأعْرَابيَّ حِمَاراً كُنْتَ تَرَوَّحُ     عَلَيهِ ، وعِمَامةً كُنْتَ تَشُدُّ بِهَا رَأسَكَ ؟ فَقَالَ : إنِّي سَمِعتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يَقُولُ : (( إنَّ مِنْ أبَرِّ البِرِّ أنْ يَصِلَ الرَّجُلُ أهْلَ وُدِّ أبيهِ بَعْدَ أنْ يُولِّيَ )) وَإنَّ أبَاهُ كَانَ صَديقاً لعُمَرَرضي الله عنه.

رَوَى هذِهِ الرواياتِ كُلَّهَا مسلم .

Imepokewa kutoka kwake 'Abdillaahi bin Diynaar  (Radhwiyah Allaahu 'anhu) Kuwa 'Abdillaahi bin 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) alikutana na Bedui katika njia ya Makkah. 'Abdillaahi bin 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) akamsalimia akampandisha kwenya punda wake aliye mpaka, akampatia kilemba kilicho kichwani mwake. Ibn Diynaar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) akasema: Tukamwambia: "Allaah Akutengeneza, Wao ni Mabedui wanaridhika na mepesi." Akasema 'Abdillaahi bin 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu): "Babake huyu alikuwa rafiki mkubwa wa 'Umar bin Al-Khatw'aab (Radhwiyah Allaahu 'anhu), nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika wema mkubwa ni kwa mtu kuunga vipenzi vya baba yake."

Katika riwaayah ya Ibn Diynaar, Ibn 'Umar (Radhiwyah Allaahu 'anhu) alikuwa anapotoka kwenda Makkah alipochoka kupanda ngamia anapumzika, kilemba anakazia kichwa chake. Alipokuwa hivyo siku moja juu ya punda, akapita bedui, akamuuliza: "Je, wewe ndiye mtoto wa fulani?" Akajibu: "Ndio." Akamtunikia punda, na kumwambia: "Mpande huyu." Na pia akampatia kilemba, kamwambia: "Kifunge kichwani mwako." Baadhi ya maswahibu zake wakamwambia: "Allaah Akughufirie, umempatia huyu bedui punda uliyekuwa ukimtumia kwa safari zako na kilemba ulichokuwa ukifunikia kichwa chako." Akasema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika wema mkubwa kabisa ni mtu kuunga vipenzi wa baba yake baada ya kufa kwake", na babake alikuwa ni rafiki wa 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu). [Zimepokewa hizi riwaayah zote na Muslim]

 

 

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي أُسَيد - بضم الهمزة وفتح السين - مالك بن ربيعة الساعدي رضي الله عنه، قَالَ : بَيْنَا نَحْنُ جُلُوسٌ عِنْدَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم إذ جَاءهُ رَجُلٌ مِنْ بَنِي سَلَمَةَ ، فَقَالَ : يَا رسولَ اللهِ ، هَلْ بَقِيَ مِنْ برِّ أَبَوَيَّ شَيء أبرُّهُما بِهِ بَعْدَ مَوتِهمَا ؟ فَقَالَ :   (( نَعَمْ ، الصَّلاةُ عَلَيْهِمَا ، والاسْتغْفَارُ لَهُمَا ، وَإنْفَاذُ عَهْدِهِمَا مِنْ بَعْدِهِما ، وَصِلَةُ الرَّحِمِ الَّتي لا تُوصَلُ إلاَّ بِهِمَا ، وَإكرامُ صَدِيقهمَا )) رواه أَبُو داود .

Amesema Abu Usayd Maalik bin Rabi'ah As-Saa'idiy (Radhwiyah Allaahu 'anhu): "Tulipokuwa tumekaa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja mtu kutoka katika ukoo wa Salimah akasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, kumebakia wema wa kuwatendea wazazi wangu baada ya kufa kwao?" Akasema: "Ndio, kuwaombea du'aa, kuwatakia maghfira, kutekeleza ahadi zao baada ya kufa kwao, kuunga kizazi ambacho hakiungiki ila kwa sababu yao na kuwakirimu marafiki zao." [Abu Daawuud]

 

 

Hadiyth – 4

وعن عائشة رضي الله عنها ، قَالَتْ : مَا غِرْتُ عَلَى أحَدٍ مِنْ نِسَاءِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم مَا غِرْتُ عَلَى خَدِيجَة رضي الله عنها ، وَمَا رَأيْتُهَا قَطُّ ، وَلَكِنْ كَانَ يُكْثِرُ ذِكْرَهَا ، وَرُبَّمَا ذَبَحَ الشَّاةَ ، ثُمَّ يقَطِّعُهَا أعْضَاء ، ثُمَّ يَبْعثُهَا في صَدَائِقِ خَديجَةَ ، فَرُبَّمَا قُلْتُ لَهُ : كَأنْ لَمْ يَكُنْ في الدُّنْيَا إلاَّ خَديجَةَ ‍! فَيَقُولُ : (( إنَّهَا كَانَتْ وَكَانَتْ وَكَانَ لي مِنْهَا وَلَدٌ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : وإنْ كَانَ لَيَذْبَحُ الشَّاءَ ، فَيُهْدِي في خَلاَئِلِهَا مِنْهَا مَا يَسَعُهُنَّ .

وفي رواية:كَانَ إِذَا ذبح الشاة، يقولُ : (( أَرْسِلُوا بِهَا إِلَى أصْدِقَاءِ خَديجَةَ )) .

وفي رواية : قَالَت : اسْتَأذَنتْ هَالَةُ بِنْتُ خُوَيْلِد أُخْتُ خَدِيجَةَ عَلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، فَعرَفَ اسْتِئذَانَ خَديجَةَ ، فَارتَاحَ لِذَلِكَ ، فَقَالَ : (( اللَّهُمَّ هَالةُ بِنْتُ   خُوَيْلِدٍ )) .

Amesema 'Aa'ishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa): "Sijamuonea wivu yeyote miongoni mwa wake wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama nilivyomuonea wivu Khadijah ilhali sijawahi kumuona kabisa Khadijah (Radhwiyah Allahu 'anhaa), lakini Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimtaja sana. Mara nyengine alikuwa akichinja mbuzi, akimkata vipande kisha akiwapelekea marafiki za Khadijah. Mara nyengine nilimwambia: "Kama kwamba hakuna duniani ila Khadijah." Akasema: "Alikuwa kadha wa kadha, amenizalia watoto." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika riwaayah nyengine: "Alikuwa anachinja mbuzi na kuwazawadia rafikize Khadijah kinachowatosha.

Katika riwaayah nyengine: "Alikuwa anapochinja mbuzi husema: "Wapelekeeni rafiki za Khadijah."

Katika riwaayah nyengine: "Haalah bint Khuwaylid, dadake Khadijah, alibisha hodi kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akamtambua hodi ya Khadijah (kwa  ile sauti), akafurahi kuja kwake, akasema: "Ee Allaah! Huyu ni Haalah bint Khuwaylid."

 

 

Hadiyth – 5

وعن أنس بن مالك رضي الله عنه، قَالَ : خرجت مَعَ جرير بن عبد الله البَجَليّ رضي الله عنه في سَفَرٍ ، فَكَانَ يَخْدُمُني ، فَقُلْتُ لَهُ : لاَ تَفْعَل ، فَقَالَ : إِنِّي قَدْ رَأيْتُ الأنْصَارَ تَصْنَعُ برسول الله صلى الله عليه وسلم شيئاً آلَيْتُ عَلَى نَفسِي أنْ لا أصْحَبَ أحَداً مِنْهُمْ إلاَّ خَدَمْتُهُ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Amesema Anas bin Maalik (Radhwiyah Allaahu 'anhu): "Nilisafiri na Jariyr bin 'Abdillaahi Al-Bajaliyy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) safarini, alikuwa ananitumikia, nikamwambia: "Usifanye hivyo." Akasema: "Mimi nimewaona Answari wakimfanyia hilo Rasuli Wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hivyo nikala kiapo kuwa kila nitakapofuatana na mmoja nitamhudumia." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share