043-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuwakirimu Watu wa Nyumba ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Kubainisha Fadhila Zao
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب إكرام أهل بيت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وبيان فضلهم
043-Mlango Wa Kuwakirimu Watu wa Nyumba ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Kubainisha Fadhila Zao
قَالَ الله تَعَالَى:
إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا ﴿٣٣﴾
Hakika Allaah Anataka Akuondosheeni maovu enyi ahli wa nyumba (ya Nabiy) na Akutakaseni mtakaso barabara. [Al-Ahzaab: 33]
وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ ﴿٣٢﴾
Na yeyote anayeadhimisha Ishara za Allaah, basi hayo ni katika taqwa ya nyoyo. [Al-Hajj: 22]
Hadiyth – 1
وعن يزيد بن حَيَّانَ ، قَالَ : انْطَلَقْتُ أنَا وحُصَيْنُ بْنُ سَبْرَة ، وَعَمْرُو ابن مُسْلِم إِلَى زَيْد بْنِ أرقَمَ رضي الله عنه، فَلَمَّا جَلسْنَا إِلَيْهِ قَالَ لَهُ حُصَيْن : لَقَدْ لقِيتَ يَا زَيْدُ خَيْراً كَثِيراً ، رَأيْتَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، وسمعتَ حديثَهُ ، وغَزوْتَ مَعَهُ ، وَصَلَّيْتَ خَلْفَهُ : لَقَدْ لَقِيتَ يَا زَيْدُ خَيْراً كَثيراً ، حَدِّثْنَا يَا زَيْدُ مَا سَمِعْتَ مِنْ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : يَا ابْنَ أخِي ، وَاللهِ لقد كَبِرَتْ سِنِّي ، وَقَدُمَ عَهدِي ، وَنَسيتُ بَعْضَ الَّذِي كُنْتُ أعِي مِنْ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، فما حَدَّثْتُكُمْ ، فَاقْبَلُوا ، ومَا لا فَلاَ تُكَلِّفُونيهِ . ثُمَّ قَالَ : قام رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَوماً فينا خَطِيباً بمَاء يُدْعَى خُمَّاً بَيْنَ مَكَّةَ وَالمَدِينَةِ ، فَحَمِدَ الله ، وَأثْنَى عَلَيهِ ، وَوعظَ وَذَكَّرَ ، ثُمَّ قَالَ : (( أمَّا بَعدُ ، ألاَ أَيُّهَا النَّاسُ ، فَإنَّمَا أنَا بَشَرٌ يُوشِكَ أنْ يَأتِي رسولُ ربِّي فَأُجِيبَ ، وَأنَا تارك فيكم ثَقَلَيْنِ : أوَّلُهُمَا كِتَابُ اللهِ ، فِيهِ الهُدَى وَالنُّورُ ، فَخُذُوا بِكتابِ الله ، وَاسْتَمْسِكُوا بِهِ )) ، فَحَثَّ عَلَى كِتَابِ الله ، وَرَغَّبَ فِيهِ ، ثُمَّ قَالَ : (( وَأهْلُ بَيْتِي أُذكِّرُكُمُ الله في أهلِ بَيْتي ، أذكرُكُمُ الله في أهل بيتي )) فَقَالَ لَهُ حُصَيْنٌ : وَمَنْ أهْلُ بَيتهِ يَا زَيْدُ ، أَلَيْسَ نِسَاؤُهُ مِنْ أهْلِ بَيْتِهِ ؟ قَالَ : نِسَاؤُهُ مِنْ أهْلِ بَيتهِ ، وَلكِنْ أهْلُ بَيتِهِ مَنْ حُرِمَ الصَّدَقَةَ بَعدَهُ ، قَالَ : وَمَنْ هُمْ ؟ قَالَ : هُمْ آلُ عَلِيٍّ وَآلُ عقيل وَآلُ جَعفَرَ وآلُ عَبَّاسٍ . قَالَ : كُلُّ هؤلاء حُرِمَ الصَّدَقَةَ ؟ قَالَ : نَعَمْ . رواه مسلم .
وفي رواية : (( ألاَ وَإنّي تَارِكٌ فِيكُمْ ثَقَليْنِ : أحَدُهُما كِتَابُ الله وَهُوَ حَبْلُ الله ، مَنِ اتَّبَعَهُ كَانَ عَلَى الهُدَى ، وَمَنْ تَرَكَهُ كَانَ عَلَى ضَلالَة )) .
Amesema Yaziyd bin Hayyaan: Mimi, Huswayn bin Sabrah na 'Amru bin Muslim tulimtembelea Zayd bin Muslim (Radhwiyah Allaahu 'anhu). Tulipokaa naye, Huswayn akamwambia: "Hakika ee Zayd, umepata kheri nyingi, umemuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), ukasikia mazungumzo yake, ukapigana pamoja naye, na ukaswali nyuma yake. Hakika umepata kheri nyingi,ee Zayd! Tuhadithie Zayd uliyosikia kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akamwambia: "Ee mpwa wangu! Wa- Allaahi, Nimezeeka, zama zangu zimepita na nimesahau baadhi ya niliyohifadhi kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Nitakacho wahadithia kipokeeni, na ambacho sikuwahadithia musinilazimishe kukizungumza." Kisha akasema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama siku moja mahali panapoitwa Khum baina ya Makkah na Madiynah; kutuhutubia, Akamuhimidi Allaah, akamsifu, akaedhea; kisha akasema: "Ama baada ya haya: Fahamuni enyi watu! Hakika mimi ni mwanadamu, anakaribia kunijia Mjumbe wa Mola wangu nami niitikie wito huo, nami nimewaachia vizito viwili: cha kwanza ni Kitabu cha Allaah, ambacho kina uongofu na nuru ndani yake, kichukueni Kitabu cha Allaah ns mshikamane nacho barabara." Akasisitiza mno juu ya kushikamana na Kitabu cha Allaah, kisha akasema: "Na watu wangu wa nyumbani, mkumbukeni Allaah kwa watu wa nyumbani kwangu." Huswayn akamwambia: "Ee Yaziyd, ni nani hao watu wa nyumbani kwake? Wake zake si ni watu wa nyumba yake?" Akasema: "Wake zake ni katika watu wa nyumbani kwake, lakini watu wa nyumba yake haswa ni wale waliokatazwa kula sadaqah baada yake." Akaulizwa: "Na ni kina nani hao?" Akasema: "Hao ni familia ya 'Aliy, familia ya 'Aqiyl, familia ya Ja'far na familia ya 'Abbaas." Akasema: "Wote hao wamekatazwa na kuharamishwa sadaqah?" Akasema: "Ndio." [Muslim]
Katika riwaayah: "Fahamuni kuwa nimewaachieni vizito na vitukufu viwili: Ya kwanza Kitabu cha Allaah, nayo ni kamba ya Allaah. Mwenye kukifuata atakuwa juu ya uongofu na mwenye kukiacha atakuwa juu ya upotevu."
Hadiyth – 2
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، عن أَبي بكر الصديق رضي الله عنه - مَوقُوفاً عَلَيهِ - أنَّهُ قَالَ : ارْقَبُوا مُحَمداً صلى الله عليه وسلم في أهْلِ بَيْتِهِ . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) kuwa Abu Bakr Asw-Swiddiq (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "Mheshimmuni na mkirimuni Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika familia yake." [Al-Bukhaariy]